SoC03 Mambo mawili ya kujenga Jamii Bora

Stories of Change - 2023 Competition

Mwalimu AKILI

New Member
May 1, 2023
1
1
Jamii,ni jumla ya watu wote wanaoishi katika mazingira Fulani ya kijiografia ambao wanaweza kufanana au kutofautiana katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, na kiteknolojia.

Kujenga maana yake kutengeneza kitu ambacho kina faida na kutumika kipindi fulani Cha maisha mfano nyumba. Kwa mantiki hii, jamii inaweza kufananishwa na nyumba. Na ili nyumba hii iweze kuwa bora inahitaji baba na mama Bora.

Vivyo hivyo ili jamii iwe Bora na yenye malengo sahihi na mipango sawia katika kuleta maendeleo chanya leo, kesho na kuendelea inahitaji Mambo makubwa mawili tu.

1. Sheria, huu Ni Utaratibu unawaongoza watu ili kukidhi mahitaji Yao muhimu. Kuna Sheria za nchi, Sheria za taasisi, Sheria za dini, Sheria za familia n.k ikiwa Sheria hizi zitaanzia nyumbani yaani kila familia iwe na Sheria za kujenga, Ni Rahisi Sana watoto watakaozaliwa kufuata Sheria popote watakapoishi kwa sababu walizoea mwongozo wa Sheria katika Maisha Yao. Mara nyingi familia yenye Sheria, nidhamu hupatikana, maadili mema Ni tabia, na hapo ndipo huzaliwa jamii Bora.

Kwani Kwa kufanya hivi jamii itakuwa yenye maadili mema na maovu mengi yatakuwa yameepukwa kwa kiasi kikubwa mpaka kwa taifa kwa ujumla. Ikiwa kila mtoto, kijana, wazee watafuata Sheria ni rahisi sana kuepukana ama kuisha kwa maovu kwa kiasi kikubwa. Shule nzuri inayoweza kutekeleza Sheria siyo mahakama Wala polisi, Bali Ni nyumbani. Naam, vile vile Jambo la Pili Ni;-

2. Uwajibikaji, Ni kitendo Cha kutimiza wajibu wa kila siku ambao MTU amejiwekea au upo kwa MTU binafsi, serikali au taasisi Fulani. Jambo hili linaweza kukamilika ikiwa Sheria imefuatwa, yaani Ni kusema kwamba Sheria na Uwajibikaji Ni vitu pacha ambavyo vinategemeana.

Kila mtu kuanzia kwenye familia hasa mtoto mdogo mpaka kiongozi mkuu wa nchi yaani Rais, akiwajibika kwa usawa na ufasaha Ni rahisi sana jamii hiyo kuwa na maadili mema yanaoondoa uvivu na uzembe usio wa lazima na mwisho wa siku, jamii itakuwa imeondoa wizi, ugomvi na vifo visivyo vya lazima katika jamii vinavyoletwa na uzembe wa kutofanya kazi ambao umeletwa na kukosekana kwa Sheria tangu mtoto akiwa kwa wazazi mpaka anapotoka mazingira ya nyumbani

Jamii haijengwi kwa watu waliokomaa tayari na Wana akili za kuwaza, ili jamii iwe Bora yenye kufuata Sheria na Uwajibikaji. Ni lazima na siyo hiari, Elimu ya umuhimu wa kutunga na kutekeleza Sheria, pamoja Uwajibikaji itolewe kwa watoto huku shinikizo likifanyika kwa wazazi kwani ndiyo chachu ya kuwafanya watoto wajue umuhimu wa Sheria na Uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom