Makalla: CCM tunaheshimu Mahakama kama chombo cha kutoa haki, hatuingilii kesi zinazosikilizwa huko

Cute Wife

Senior Member
Nov 17, 2023
153
390
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaheshimu mhimili wa Mahakama na katika usikilizaji kero za wananchi, viongozi wa chama hicho hawatajihusisha na kesi zilizopo mahakamani.

Makalla ameyasema hayo leo Jumanne Mei 7, 2024 akifanya mahojiano maalumu na waandishi na wahariri wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea ofisi za kampuni hiyo, Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

"Naulizwa mtangulizi wako hakuamini Mahakama na wewe unasema mnaiamini, je, tuchukue lipi? Chukueni kauli ya kwangu kwamba Chama cha Mapinduzi na Serikali yake inaheshimu Mahakama kama chombo cha kikatiba cha kutoa haki. Niwashauri wananchi kama jambo lipo mahakamani ukishindwa kata rufaa katika ngazi inayofuata," amesema.

Mwananchi

====

Pia soma:

-
Makonda kusikiliza kero zenye kesi Mahakamani Arusha, asema yupo tayari kupoteza chochote mradi mtu apate haki yake

- Makalla atua Katavi na kusema Watasikiliza kero za Wananchi lakini siyo zile zilizopo Mahakamani
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaheshimu mhimili wa Mahakama na katika usikilizaji kero za wananchi, viongozi wa chama hicho hawatajihusisha na kesi zilizopo mahakamani.

Makalla ameyasema hayo leo Jumanne Mei 7, 2024 akifanya mahojiano maalumu na waandishi na wahariri wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea ofisi za kampuni hiyo, Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

"Naulizwa mtangulizi wako hakuamini Mahakama na wewe unasema mnaiamini, je, tuchukue lipi? Chukueni kauli ya kwangu kwamba Chama cha Mapinduzi na Serikali yake inaheshimu Mahakama kama chombo cha kikatiba cha kutoa haki. Niwashauri wananchi kama jambo lipo mahakamani ukishindwa kata rufaa katika ngazi inayofuata," amesema.

Mwananchi
Anaongea hayo ingali leo wamezindua namba maalum ya kuoiga simu kuhusu ile waliyoita Samia helpline ya kusikiliza kero za wananchi na kutoa legal aid? Hii maana yake nini? Stupid.
 
Acha kutueleza sisi, hebu mpgie simu mweleze jamaa yako pale Ngaranaro ndo tutaamini kweli wewe ni "KIDUME"...
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaheshimu mhimili wa Mahakama na katika usikilizaji kero za wananchi, viongozi wa chama hicho hawatajihusisha na kesi zilizopo mahakamani.

Makalla ameyasema hayo leo Jumanne Mei 7, 2024 akifanya mahojiano maalumu na waandishi na wahariri wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea ofisi za kampuni hiyo, Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

"Naulizwa mtangulizi wako hakuamini Mahakama na wewe unasema mnaiamini, je, tuchukue lipi? Chukueni kauli ya kwangu kwamba Chama cha Mapinduzi na Serikali yake inaheshimu Mahakama kama chombo cha kikatiba cha kutoa haki. Niwashauri wananchi kama jambo lipo mahakamani ukishindwa kata rufaa katika ngazi inayofuata," amesema.

Mwananchi
Hawa jamaa wamefeli Kila idara
 
Anaongea hayo ingali leo wamezindua namba maalum ya kuoiga simu kuhusu ile waliyoita Samia helpline ya kusikiliza kero za wananchi na kutoa legal aid? Hii maana yake nini? Stupid.
Makalla Mjinga Fulani hivi

Kero za wananchi ziko kwenye mihimili yote ikiwemo mahakama .Kazi ya chama tawala ni kudikiliza kero za wananchi na kuzitafitia ufumbuzi ikiwemo kutoa msaada wa kisheria au kuzipeleka Kwa uongozi wa mahakama

Uongozi wa mahakama utajuaje kama Kuna kero Kwa wananchi

Chama tawala ndio kazi yake

Aseme yeye binafsi ndie hatapokea hizo kero
 
We ndo mjinga
Nchi inaongozwa kwa taratibu na sheria zilizotungwa bungeni
 
Taratibu Gani watu wanalia
wapi unataka watu walalamike wapi?

Kwa taarifa Yako mahakimu kibao wameshawajibishwa na mahakama baada ya wananchi kulalamika Kwa Makonda na ikathibitika kweli

Mihimili wa mahakama pia Kuna watu wanachemka huko .Na wananchi mashahidi .Hakuna Cha kujiificha nyuma ya chaka au joho la kijaji kuwa kesi hii Iko mahakamani wakati Kuna uhuni

Wacha wananchi watapike nyongo zao itasaidia mahakama kunyooka wakijua wakicheza wataumbuliwa mchana kweupe na wananchi Bila woga Wala Nini

Ni wake up call Kwa mihimili wa mahakama

Makonda endelea kusikiliza kero za wananchi zikiwemo kero za mhimili wa mahakama
 
Nakubaliana na Makalla kwenye hili. Jambo kama lipo mahakamani, sawa-tena ni dharau kwa mahamaka, kulijadili na kulitolea maamuzi ya kisiasa. Hata utekelezaji wa hukumu za mahakama huratibiwa na mahakama kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.

Kujadili na kutoa maamuzi ya kisiasa juu ya masuala yaliyopo mahakamani kunaweza: mosi, kufitinisha mahakama na wananchi. Pili, kuwapa viongozi wa kisiasa kazi ambazo hawana kikatiba na kisheria. Tatu, kuonesha na kuleta nadharia kuwa mambo yanayoanzia mahakamani humalizika kisiasa.

Awe Makonda au yeyote yule, iwe marufuku kuchanganya siasa na mambo yaliyopo mahakamani.
 
Chukueni kauli ya kwangu kwamba Chama cha Mapinduzi na Serikali yake inaheshimu Mahakama kama chombo cha kikatiba cha kutoa haki.

Kada na mfadhili wa chama dola kongwe pia rafiki wa viongozi wa juu wa chama tawala na serikali alisema waziwazi :

1715794157226.png

Nakubaliana na Makalla kwenye hili. Jambo kama lipo mahakamani, sawa-tena ni dharau kwa mahamaka, kulijadili na kulitolea maamuzi ya kisiasa. Hata utekelezaji wa hukumu za mahakama huratibiwa na mahakama kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.

Kujadili na kutoa maamuzi ya kisiasa juu ya masuala yaliyopo mahakamani kunaweza: mosi, kufitinisha mahakama na wananchi. Pili, kuwapa viongozi wa kisiasa kazi ambazo hawana kikatiba na kisheria. Tatu, kuonesha na kuleta nadharia kuwa mambo yanayoanzia mahakamani humalizika kisiasa.

Awe Makonda au yeyote yule, iwe marufuku kuchanganya siasa na mambo yaliyopo mahakamani.
Fani mbili zinazoongoza kulalamikiwa na wananchi kitaifa Kwa uovu ziko mbili Idara ya Ardhi na mahakama

Hao ndio vinara wanaongoza kulalamikiwa na wananchi

Kesi kuwa mahakamani sio Kichaka Cha kukitumia Kwa maovu.Mtu kesi imeisha kutoa tu hati ya judgement inachukua mwaka mzima mtu anafuatilia hapati wanataka rushwa unatakaje mtu akae kimya asiongee kuwa huko kumeoza kesi Ina mwaka Toka iamuliwe nakala ya hukumu haitoki
 
Back
Top Bottom