Madhara ya maamuzi kutolewa na mtu mmoja

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Tuliandika hapa madhara ya mtu mmoja kuamka na kutoa maamuzi ya Taasisi kama alivyofanya Zitto Kabwe kwenye suala la kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji.

Zitto alifuata mkumbo wa CHADEMA ambao kiuhalisia wao walikaa kikao Dodoma na kuamua, Zitto alikaa na nani?

Lipumba ajitahidi kuukwepa huo mtego, walijipa muda wakakutana na kutoka na maamuzi.

Mpaka hapo utaona CUF na CHADEMA walifuata katiba za vyama vyao kufanya maamuzi ila Zitto alitumia mahaba yake kwa Mbowe kifuata mkumbo.

Matokeo yake Wagombea wa ACT wameamua kufanya zao kampeni maana Chama hakijaamua bali aliamua Zitto Kabwe kutoshiriki.

Hongereni sana wagombea mnaoendelea kujitambua.

IMG-20191118-WA0034.jpeg
 
Back
Top Bottom