Stories of Change - 2023 Competition

Mathew Leloo

New Member
Jul 18, 2022
2
4
Katika mada yetu mwaka huu, kama we ni kiongozi jiulize maswal adilifu, nini maana ya uadilifu? Je, Kama viongozi, mnaongoza watu wenu kwa uadilifu? Je, nini hutokea kiongozi Anapokosa uadilifu?

Jiulize maswal adilifu:

• Je, ninashuku kwamba kitendo Fulani kinaweza kuwa cha haramu au kisichokuwa cha maadili?

• Itaonekana aje kama uamuzi huu utaripotiwa kwa gazeti, au kama nitaongea kuhusu jambo hili na familia yangu na marafiki?

• Je, kitendo kinachopendekezwa kinahusu udanganyifu au kutokuwa na ukweli?

• Je, kitendo kinachopendekezwa kinaweza kuhatarisha usalama au afya ya mtu binafsi au watu wengine?

• Kitendo kinachopendekezwa kinaweza kuharibu sifa yangu?

• Kitendo hicho kiko na madhumuni ya uongozi yaliyohalali?

Kama kitendo kinachopendekezwa hakitafaulu jaribio lolote la majaribio haya, lazima utafute ushauri na ufikirie tena uamuzi wako.

Katika harakati za kujenga utawala bora katika uongozi wowote ni lazima uadilifu na uwajibikaji uwepo ili kuhakikisha malengo na matarajio ya kuongoza kidemokrasia yanatimia.

Ni matumaini yangu kuwa dhana ya neno Uadilifu inaeleweka kwa kiasi fulani na ndio maana wananchi wanaweza kuwatofautisha walio waadilifu na wasio waadilifu katika uongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya juu katika serikali. Lakini kwa faida ya wasomaji wengine ambao wanataka kujua uadilifu katika uongozi ukoje, ngoja nianze na dhana ya Uadilifu.

Uadilifu ni hali ya kutenda haki pasipo kufanya upendeleo kwa upande fulani, kuwa mwaminifu kwa wale unaowaongoza na kutokumbatia matumizi mabaya ya madaraka ambayo kiongozi anayo. Na uongozi ambao unafuata misingi ya haki na sheria pamoja na kuizingatia kikamilifu, huo ndio tunaouita Utawala bora.
Katika uongozi wowote ambao una utawala bora ndani yake ni lazima kuwepo na mambo yafuatayo;

• Utawala unaozingatia sheria
• Viongozi huwa ni wawajibikaji kwa wanaowaongoza.
• Viongozi kuwa wakweli na uwazi unakuwepo katika uongozi huo.
• Vyombo vya habari vinapewa uhuru pasipo kuviwekea vikwazo katika shughuli zao.
• Kuzingatia haki za binadamu na kuzilinda kwa kiasi kikubwa

Endapo mambo hayo yatafanyika na kuzingatiwa katika uongozi, basi hapo ndipo tunaweza kusema kuwa Uongozi wa wale wanaowaongoza wengine ni wa kidemokrasia yaani kwa maana nyingine ni kwamba kuna utawala bora katika uongozi huo.

Lakini kama nilivyoanza kuandika makala hii kule juu katika kichwa cha habari nilisema kuwa Hakuna utawala bora pasipo uadilifu na uwajibikaji kwa sababu kama viongozi wetu wakipuuza kwa makusudi uadilifu na uwajibikaji katika uongozi basi watakuwa wamebeba dhamira ya kuuchukia, kuupoteza au kuuzika kabisa utawala bora. Na ukiona ukiukwaji huu wa kuongoza nchi kidemokrasia unaepukwa, basi ujue kuwa viongozi hao ambao dhamana ambayo wanayo aidha ni wamepewa na uongozi wa juu au wamechaguliwa na wananchi hawana dhamira ya dhati ya kutaka kufanya utawala wa kidemokrasia ulio bora.

Kama tumejua kwamba hakuna utawala bora pasipo kuwa na utayari wa Uadilifu na uwajibikaji, basi kuna vitu au mambo ambayo ni lazima yafanyike kwa viongozi ili kudumisha Uadilifu katika utawala ulio bora.
Mambo yanayoimarisha uadilifu na uwajibikaji katika utawala bora.

• Matumizi mazuri ya uongozi. Kiongozi yeyote ambaye ni muadilifu hutumia mamlaka yake vizuri kwa kutoa huduma kwa wananchi wake pamoja na kuufanya uongozi wake kuwa wa kisheria na unaoheshimu matakwa ya wananchi wake ambao wamempa dhamana ya kuwa kiongozi.

• Uaminifu. Katika mambo muhimu ya kuyazingatia kwa kiongozi muadilifu ni pamoja na hili la kuwa mwaminifu kwa jamii ambayo anaiongoza. Endapo kiongozi huyo atakuwa mwadilifu atakuwa anajijengea heshima na jamii itakuwa na imani na serikali kwa ujumla. Ili utawa bora udumishwe, sharti viongozi wawe waaminifu kwa kila jambo wanalolisimamia.

• Matumizi mazuri ya misingi ya sheria. Sheria zote ambazo zimekuwa zikiongoza nchi na ambazo zimewekwa na jamii ndizo zitamfanya kiongozi muadilifu kudumisha utawala bora. Ni vibaya sana na ni lazima likemewe endapo kiongozi kwa namna yoyote ile atajaribu kupindisha misingi ya sheria kwa sababu ya kutaka mtu, kikundi au jamii fulani ipewe kipaumbele (upendeleo).

• Ukweli na uwazi katika uongozi. Uadilifu wa kiongozi yeyote unaonekana pia kwa yeye kuwa mkweli na muwazi kwa halaiki ya watu ambao anaowaongoza. Endapo kiongozi atakuwa mkweli na muwazi atawatoa wasiwasi wananchi na kuondoa hisia mbaya kwao (wananchi) dhidi ya uongozi wake.

Kwakusema hayo, endapo uadilifu na uwajibikaji ukizingatiwa katika suala zima la uongozi basi mfumo mzima wa uongozi kuanzia ngazi ya chini na kuendelea, utakuwa bora na wananchi watakuwa na imani isiyoyumbayumba juu ya viongozi wao. Ikumbukwe kuwa siku zote halaiki ya wananchi wanakuwa na imani na viongozi wao kama tu watakuwa hawaoni viongozi wao wanapotosha maadili ya uongozi kwa kufanya mambo ambayo yanaweza kupotosha maadili ya uongozi kama vile; kuomba na kupokea rushwa, kufanya ubadhirifu na ufujaji wa mali ya umma, kutumia vibaya madaraka na kadhalika. Ikumbukwe “viongozi mtuongozeni Kwa iman na amani”.
 
Back
Top Bottom