Kuanzia mashabiki, uongozi na mwisho wachezaji wa Simba,utaona kuchanganyikiwa kusiko na kipimo (beyond measure). Wenzao Yanga wametulia tuli.
Simba wanafikiri kuwa na jina kubwa ni magoli tayari. Wanafikiri tambo za msemaji na mashabiki wakereketwa ndio kuongeza umahiri wa wachezaji. Wanafikiri uchambuzi wa wachambuzi wetu uchwara, unaakisi hali halisi ya timu. Kwa ufupi, Simba huwa wanaingia uwanjani wakidhani wameishashinda, kumbe mchezo bado. Kwa hiyo matokeo yakiwa tofauti na yale waliyolala nayo, wanatamani kujiyonga.
Tumeona jana wachezaji wetu walivyo wazito. Ni wazito kiasi kwamba, eti Kibu ndiye tegemeo. Na ile penati, washukuru mchongo wa MO.
Hivi tujiulize, ni mchezaji gani ambaye tumemsajili kwa kushindana na timu nyingine. Labda tu Ngoma ambaye 'tulimuiba' airport. Lakini Chama tumemrudisha baada ya kuwa zigo huko alikokuwa. Konde Boy hivyo hivyo. Matokeo tunayaona.
Hawa kina Beleke, Onana, Phiri n.k.,hatujawahi kuwasikia kokote. Wamepambwa umaarufu baada ya kuja Simba, ili kuwahalalisha. Kumbe hamna kitu. Hivi kweli hapo kuna ushindi?
Hakika Simba inahitaji mapinduzi kifikra na kimtazamo.
Mlale unono