Kwa Milioni 30, UTT amis na nyumba ya kupangisha kipi bora?

Utt amis ni soko la hisa,
Hisa sokoni zinaweza kupanda au kushuka unatakiwa ulijue hilo,na ulielewe
Usije ukaleta fujo,siku unaambiwa mil 10 yako thamani yake imeshuka mpaka 4m.
Utt amis ni vpande vya mutual fund na sio soko la hisa (Share).

#YNWA
 
Haiwezekani niweke mil 30 halafu mnipe 250k kila mwezi.
Hizi mambo zinawafaa wavivu au wastaafu
Mimi hapa ndio nashindwa kuelewa watu wanatumia ubongo au mavi kufikiria, swali la kwanza kujiuliza huyu mtu mil 30 ameitoa wapi mpaka aieweke asubiri 250k … Kweli mtu mvivu anaweza kuwa na mil 30 ?
 
Mimi hapa ndio nashindwa kuelewa watu wanatumia ubongo au mavi kufikiria, swali la kwanza kujiuliza huyu mtu mil 30 ameitoa wapi mpaka aieweke asubiri 250k … Kweli mtu mvivu anaweza kuwa na mil 30 ?

Si ndio hapo cha msingi kwenye maisha kila mtu na fikra zake.
Namshangaa na simuelewi mtu anayekandia uwekezaji kwenye real estate hususani rental premises.
Ukiona mtu anafanya hivyo seriously usimchukulie poa.
Ndio maana siku hizi kuna trend matajiri wengi wa ma hardware ma daladala wana venture kwenye kuinvest kwenye rental premises
 
Tunaweza kutofautiana kimtazamo lakini ukweli unabakia pale pale, kwa Tanzania yetu hii, ukiondoa uwekezaji kama wa UTT, karibu biashara zingine zote ni pasua kichwa. Usipoibiwa na watu, utafirisiwa na Serikali. Utitiri wa makodi, matozo na blah blah kibao.
Hiyo UTT haina connection na hii serikali? Yasije tokea mambo NHIF wanakopa ela hawarudishi?
 
Hivi unajua kuwa UTT AMIS ni taasisi iliyopo chini ya wizara ya fedha? Unaanzaje kuifananisha na DECI au hauna taarifa jinsi gani inaoperate na aina ya mifuko yake? Kuwa na taarifa boss.
Sasa wewe ndiye ungeleta taarifa sahihi sio kuimba taarabu. Je hiyo UTT haina connection na serikali?
 
Hivi huwa mnawezaje kuwaza kupata pesa kiasi fulani kikubwa kuliko uwezo wa akili zenu?

Kama umeipata kwa kubeti basi endelea kubeti hadi iishe au utapata nyingine.

Milioni 30 uwekeze kwenye faida ya laki 3, (yaani 1%).... huu ni udumavu wa ubongo.

Nipatie 10M tu nikuletee laki tano kila mwezi, hapo tumegawana faida.
Unashangaa nini mkuu? Sio kila mtu ana akili ya Biashara,wengine ni waajiriwa,mishahara minono na mtu anajua kutunza pesa,katunza kapata 30m.
 
Million 10, utt Amis faida yake ipoje kwa mwezi au mwaka na ni mfuko upi bora kuwekeza
 
Salaaam Wachumi

Rejea mada hapo juu
Je upi ni uwekezaji ulio bora endapo katika harakat zako za utafutaji ukajaaliwa umeishika 30Mil cash
Na option ukawa umeweka ni hizo mbili kati ya kuwekeza utt amis ambapo kwa utafiti niliofanya humu return yake yaweza kuwa 250k-300k per month
Na kujenga nyumba ya kupangisha ambapo return yake kwa uwekezaji wa 30Mil naamin pia wazoefu watatoa muangaza
Nb/ katika ujenzi wa nyumba tuna assume kiwanja bado

JE NI UPI UWEKEZAJI ULIO BORA KATI YA HIVYO KWA MTAZAMO WAKO?
kwenye hiyo m30 toa sio zaidi ya milioni 2 kwa ajili ya biashara.
milioni 28 iliobaki jenga nyumba.
Asikushauri mtu hiyo pesa yote kuingiza kwenye biashara, Utakuja kulia kuliko mtu alofiwa na mzazi wake.
 
kwenye hiyo m30 toa sio zaidi ya milioni 2 kwa ajili ya biashara.
milioni 28 iliobaki jenga nyumba.
Asikushauri mtu hiyo pesa yote kuingiza kwenye biashara, Utakuja kulia kuliko mtu alofiwa na mzazi wake.
😃😃😃😃😃 Atalia uku anacheka
 
Jenga nyumba utakula mafao mpaka unazeeka
Anaweza kujenga,ila akili nzuri ni kuizalisha ifike kama 100M. Then, akiitoa hiyo 30 akajenga its ok anabaki na cash nzuri ambayo anaweza kufikiria sasa issues kama UTT. Nina maana, kwa hiyo hela unaweza kufanya vyote viwili endapo utavuta subira.
 
Back
Top Bottom