Kuna ndoto tatu niliota zilinistaajabisha sana

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,928
3,653
Ndoto ya kwanza
Niliota mimi flani nimezaliwa mwaka 1800's na ukijimlisha miaka 100 ni miaka ya 1900's ndo utapata mwaka niliozaliwa hii ndoto niliota kwa msisitizo mkubwa sana na ilinistaajabisha sana

Ndoto ya pili
Niliota niko sehemu ila kuna nyoka wengi wametapakaa kila mahali najaribu kuwakwepa ila hawaishi
Nyingine natembea barabarani nyoka wengi sana wamefariki na wengine wapo kwenye kuta za nyumba wanakimbia
Nyingine sekondari niliosoma kuna nyoka wengi kwenye uwanja wa mpira ila hawanioni wapo tu na shughuli zao ila mimi nawapita huku naogopa

Ndoto ya tatu
Nipo mtoni nanawa miguu nikaondoka nilipofika mbele nikakumbuka nimesahau ndoo na baadhi ya vitu nikarudi ila kufika mtoni nikawa na hofu kubwa sana nikachukua ndoo vile vitu vingine havipo nikarudi nilipotokea mbele nikawa namkaribia mtu flani analima simjui ghafla yule mtu akatupa jembe akawa anahamaki kule mtoni nilipotokea nikaona nigeuke nikaona kitu kama diamond kinameremeta sana kinanifuata ikawa imefika asubuhi nikashtuka ila ilinishangaza sana
 
Kulainisha hizo ndoto hakikisha unakula mlenda kabla ya kulala!
 
Back
Top Bottom