DOKEZO Kuna dalili ya upigaji wa Fedha za SACCOS za Wafanyakazi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Waziri Nape tusaidie

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Siku chache baada ya mmoja wa Wafanyakazi mwenzetu kuripoti juu ya madudu yanayoendelea ndani ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) inayojihusisha na uchapaji wa magazeti ya Habari Leo, Daily News na Spoti Leo, leo nami nimeona nije na hoja kadhaa kwa faida ya wenzangu.

Kwanza kabla sijaenda kwenye mada yangu, kilichotokea baada ya lile andiko kuhusu uwajibikaji wa baadhi ya viongozi kutowalipa inavyotakiwa Waandishi Vibarua (correspondent) na wale ambao wana ajira ya Mkataba, uongozi uliamua kutembeza barua kama zote kusitisha ajira za Wafanyakazi.

Waandishi wote waliokuwa vibarua kama nilivyobainisha hapo juu correspondent wa Dar es Salaam, wote walipewa barua za kutakiwa kutoendelea na majukumu yao, wale wenye ajira ya Mataba ambao ajira zao zimeifika mwisho na wanaoelekea ukingoni wote wamepewa barua za kutoendelea na utumishi.

Bahati iliyobaki ni wale ambao wana ajira ya Serikali wao ndio wameendelea kubaki, kwa ufupi uongozi ulipohojiwa kuhusu malipo ya correspondent, umeamua kufukuza kazi watu wengi kutoka idara tofautitofauti badala ya kushughulikia changamoto.

Mwaka huu tunaelekea kwenye uchaguzi, magazeti ya Serikali yanatakiwa kuwa sehemu ya kuipa nguvu Serikali na Wananchi kwa jumla kuhusu suala hilo la Kidemokrasia, lakini ndio kwanza Wafanyakazi wanafukuzwa.

Waziri Nape Nnauye hii ni Wizara yako na kizuri zaidi ni taasisi ambayo ipo chini yao kwa ukaribu zaidi, upo kimya na TSN inaelekea kuanguka na kufikilisika kabisa.

Wito wang utu kwa Nape ni kuwa aiangalie TSN kwa jicho la utofauti, kama nyumbani kwake kunawaka na nguvu zinaelekezwa kwa taasisi nyingine, basi ajue kuwa anawapa nafasi watu wengine waendelee kuinyonya TSN wanavyotaka.

Fedha za SACCOS
Nije kwenye hoja yangu ya msingi, sisi Wafanyakazi wa TSN ambao ni watumishi wa Serikalini tuna SACCOS yetu hapo, kila anayeingia anaambiwa achague kiwango cha fedha cha kukatwa.

Miaka inazidi kukatika baadhi yetu tunadai hadi shilingi Milioni 15 na zaidi lakini SACCOS imebaki kama jina tu, hakuna mikopo hatujui hela zinapoelekea, ukiuliza unaonekana ‘mnoko’.

Hizo ni fedha zetu, wengi wetu tunashindwa kukomalia kwa kuwa mazingira ya kazi za Serikalini kuna kukomoana sana, hasa ukigusa maslahi ya baadhi ya watu wenye makali.

SACCOS yetu tunakatwa hela kila siku, wapo baadhi ambao wameshastaafu lakini nao kila wakifuatilia fedha zao wanapigwa chenga, hatupewi hesabu ya akaunti ya SACCOS na hatujui nani ambaye anatoa fedha au anahifadhi fedha ambazo wafanyakazi tunakatwa.

Viongozi wetu wa juu Serikalini waiangalie TSN na uongozi wa hapo, hii fukuzafukuza ya Wafanyakazi ni kutaka kufunika mambo kama hayo niliyoyataja.
 
Back
Top Bottom