Kumfukuza Nabi ni kumwonea, tatizo la Yanga hili hapa

Sella turcica

Senior Member
Oct 13, 2020
104
194
Kwanza kabisa niwape pole wale wote wanaopenda mpira ila kwa bahati mbaya wakajikuta wanaishabikia Yanga. Nataka niwaambie wazi kuwa Yanga sio timu ya mpira bali ni kikundi cha propaganda, hata mkinitukana sawa tu ila ukweli ndiyo huo.

Timu imejaa ujanja ujanja na ukanjanja mwingi. Uwekezaji ndani ya uwanja kiduchu halafu nje ya uwanja uwekezaji kedekede. Wachezaji wanapewa sifa ambazo hawana, nikikumbuka Aucho anaitwa daktari wa mpira nacheka sana.

Sijui kama wachambuzi wengi ni mashabiki wa Yanga au wanalipwa ila wamekuwa hawatoi critical analysis kuhusu Yanga. Wanawaaminisha mashabiki wa Yanga kuwa timu iko vizuri wakati kiuhalisia sio kweli hata kidogo.

Mambo yasipokuwa shwari kule simba watasema sana, nyeupe wataita nyeupe, nyeusi itaitwa nyeusi. Bahati nzuri uongozi wa Simba umekuwa ukichukua feedback na kuifanyia kazi leo tuna confidence ya kwenda kwa mkapa kujaza uwanja kuiangalia simba ikicheza na timu yoyote nje ya Tanzania.

Hali haiko hivyo kwa Yanga. Yanga wana timu mbovu ila hawataki udhaifu wao uonekane. Wachezaji wao asilimia kubwa ni finished players. Wale wakongo waliokuwa AS vita ambayo ilipigwa na Simba nje ndani ndo wanasajiliwa eti wakapambane kimataifa kweli?

Unamsajili Morrison ili uachieve nini? Kambole kacheza misimu miwili kafunga goli mbili halafu ndo anasajiliwa, kweli? Haya huyo Kisinda kilichomrudisha ni nini? Mbio zisizokuwa na manufaa, harakati za pimbi. Eti Bigirimana amecheza EPL hahahaaa.

Kama umefuatilia vizuri ligi ya ndani utaona jinsi timu zinavyoikamia simba. Yaani simba hapati ushindi wa mseleleko, timu zinapambana kufa na kupona na hata wakifungwa wanaumia sana. Ila wakicheza na yanga huoni ile spirit ya kupambana, na wakati mwingine wameonekana kufurahia kupoteza dhidi ya Yanga, no wonder hadi sasa Yanga hajafungwa!

Kuna tuhuma kuwa jamaa wananunua mechi, well, ni tuhuma, hazijathibitishwa, ila performance ya Yanga kimataifa inaonyesha kuna ukweli katika hilo. Siku ile Vipers wamewadungua mbili bila majibu ilikuwa assessment tosha kuwa Yanga bado haina timu.

Lakini viongozi walifanya nini baada ya pale? Walipiga chini International friendlies ili udhaifu wao usionekane, wakawa wanacheza na vitimu vya ndondo huko kigamboni kimya kimya wanajipigia wanafurahi.

Preseason yenyewe vioja. Ukiwauliza wanakwambia mbona kolo anaenda Egypt ila akija tunajipigia. Yaani jamaa ni kama wanajichua vile. Ikija real performance against champions chali, pumzi hamna, wachezaji wanaruka ruka tu kama njegere kwenye sufuria.

Naamini Aziz Ki hapo alipo anajuta. Yani all the way from Ivory Coast kuja kupambana na KMC? Sijui usajili wa huyu jamaa uligharimu sh ngapi but unalipa mishahara mikubwa vile ili uchukue NBC, ambayo zawadi yake ni 600M, really?

Tuje kwenye hoja ya msingi. GSM ni nani pale Yanga? Mchakato wa mabadiliko umefikia wapi? Unakuta shabiki wa Yanga anahoji billioni 20 za Mo ila hawezi kuhoji uhalali wa GSM pale Yanga. Najua hamuwezi kumfanya kitu kwa sababu mna njaa.

GSM kaichukua ile team kwa maslahi yake binafsi. Ndiyo maana amewaletea kina Hersi na Manara halafu upande wa wachezaji anawaletea finished players. Ushindi wenu utabaki kumfunga Simba na kuchukua NBC basi. Hadi sasa Nabi ametimiza malengo yake kwa asilimia 200 na sioni sababu ya kuachana naye.

Narudia tena, Yanga ni kikundi cha propaganda. Kama kuna mchezaji mwenye malengo ya kufika mbali kicareer aende Simba. Simba ni timu yenye maono na kwa kiasi fulani ukanjanja umepungua. Jana tumeona simba queens ikisakata soka safi kule Morocco japo walichezea sana nafasi, naamini mwalimu atalifanyia kazi.

Poleni sana wapenda soka mliojikuta mnashabikia Yanga, poleni sana.
 
Dah,insha halafu hakuna kitu,yanga wanaibomoa tu Simba kila wanapokutana kwa kutumia hao hao finished players,kwa tz hakuna timu ya kuifunga yanga
Very true, mtafikisha unbeaten hata 200. But linapokuja suala la real performance ndo ukweli unadhihirika.
 
IMG-20221103-WA0514.jpg
 
Hapo kwenye Yanga kujichua hapo tatizo lipo hapo...yani raha wanajipa wenyewe bila kuangalia mashabiki wengine wanataka nini.
Yanga wenye akili kwa sasa huwasikii wakijisemesha eti un beaten wakt mpk watt wadogo wanajua mnabebwa,Yanga wenye akili wanataka timu ifanye vizuri kwenye michuano ya kimataifa timu ifahamike wachezaji wajiuze na sio ujinga wa unbeaten za droo yani 0-0,1-1 nyingiiiii bora ingekua unbeaten ya kuwafunga wanaocheza nao na wao wakiondoka na clean sheat kumbe utopolooo.
 
Hapo kwenye Yanga kujichua hapo tatizo lipo hapo.
Yanga wenye akili kwa sasa huwasikii wakijisemesha eti un beaten wakt mpk watt wadogo wanajua mnabebwa,Yanga wenye akili wanataka timu ifanye vizuri kwenye michuano ya kimataifa timu ifahamike wachezaji wajiuze na sio ujinga wa unbeaten za droo yani 0-0,1-1 nyingiiiii bora ingekua unbeaten ya kuwafunga wanaocheza nao na wao wakiondoka na clean sheat kumbe utopolooo.
Umekaza makalio ili uje uongee huu ujinga,kweli makolo mmepaniki
 
Umekaza makalio ili uje uongee huu ujinga,kweli makolo mmepaniki
Waliopaniki ni nyie wala mihogo mnaotaka kufukuza kocha na uongozi wote. Hamna akili kabisa hamtaki kuambiwa ukweli. Hakika nyie ni nyani tu
 
Kuna Wana utopolo juz tu wakawa wnaatusema et Simba ni watu wa kulia Lia Sana ,ajabu Jana kutoa draw tu kelele kila Kona ya nchi et hatumtak nabi.
Uto mna ujinga mwingi et Prof nabi sijui doctor wa mpira ,yaan Aucho akawe doctor wa mpira kweli!!
Ujanja janja wenu unawaweka uchi kimataifa .
Nyie endeleen kuwadanganya mashabaik oya oya wenu na unbeaten ya mchongo na mmekomalia hicho kipengele km njia ya kuwazuga washabik wenu.
Alafu ni ajabu mnajiita wakubwa alafu Jana mashabik wameogopa kwenda kwa mkapa ,uwanja ulikuwa mweupe had sio poa
 
Kuna Wana utopolo juz tu wakawa wnaatusema et Simba ni watu wa kulia Lia Sana ,ajabu Jana kutoa draw tu kelele kila Kona ya nchi et hatumtak nabi.
Uto mna ujinga mwingi et Prof nabi sijui doctor wa mpira ,yaan Aucho akawe doctor wa mpira kweli!!
Ujanja janja wenu unawaweka uchi kimataifa .
Nyie endeleen kuwadanganya mashabaik oya oya wenu na unbeaten ya mchongo na mmekomalia hicho kipengele km njia ya kuwazuga washabik wenu.
Alafu ni ajabu mnajiita wakubwa alafu Jana mashabik wameogopa kwenda kwa mkapa ,uwanja ulikuwa mweupe had sio poa
Nani aende kujiaibisha pale uwanjani? Wanajua namna ushindi wao unapatikana ndo maana jana hawakwenda.
 
Upepo ukivumq nyeti za kuku hubaki nje...haya ndo yanajitokeza hapo utopoloni..uhalisia utabakia vilevile...janja janja haina nafac kimataifa
 
Back
Top Bottom