SoC03 Kuelekea siku ya watu wenye ualbino duniani; Tokomeza saratani ya ngozi kufikia haki, utu na ustawi wa watu wenye Ualbino

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Changamoto za Upelelezi ,dhana duni za kutunzia ushahidi,kutokuwajibika kwa baadhi ya polisii na mahakama na kushindwa kuyalinda maeneo yalipotokea matukio kwa ajili ya ushahidi ni baadhi ya changamoto nyingine zinazokwamisha juhudi ya kupambana na makosa ya jinai nchini.

Ucheleweshaji wa vinasaba(DNA) yanayomhusisha mtuhumiwa na uhalifu alioutenda na umbali wa ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali na wilayani kulikotendeka kosa.Jeshi linakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa maabara ya uchunguzi wa kisayansi wa makosa ya jinai “forensic” na wataalamu waliosomea forensic.Hii changamoto ipo pia kwenye makosa mengine ya jinai licha ya haya yaayowahusu Albino” maneno hayo Alizungumza SSP Ramadhani Kingai katika makao makuu ya polisi Dar es salaam.

Ualbino unatofautiana hauambukizi unarithiwa kijenetiki kwa kuzaliwa. Takribani aina zote za ualbino, kama wazazi wote wawili hubeba jeni hii kuna uwezekano mkubwa kupata mtoto albino, hata kama wao hawana ualbino. Hali hiyo hupatikana kwa jinsia zote bila kujali kabila na katika nchi zote za dunia. Ualbino husababishwa na ukosefu wa rangi (melanin) katika nywele, ngozi na macho, na kusababisha kuathirika kwa mwenye ualbino kwenye jua na mwanga mkali. Kwasababu hiyo, karibu watu wote wenye ualbino wana ulemavu wa macho na wana uwezekano wa kupata saratani ya ngozi. Hakuna tiba ya ukosefu wa melanini ambayo ni kitovu cha ualbino.

Ukosefu wa melanini inamaanisha kuwa watu-wenye-ualbino wako katika hatari kubwa ya kupata saratani ya ngozi. Katika baadhi ya nchi, watu wengi-wenye -albino hufa kutokana na saratani-ya -gozi kati ya umri wa miaka 30 na 40. Saratani-ya-ngozi inaweza kuzuilika sana wakati watu-weny- ualbino wanafurahia haki yao ya afya. Hii ni pamoja na ufikiaji wa ukaguzi wa kawaida wa afya, mafuta ya kuzuia jua, miwani ya jua na nguo zinazokinga jua. Katika idadi kubwa ya nchi, njia hizi za kuokoa maisha hazipatikani au hazipatikani kwao.

Kwahiyo, katika nyanja ya hatua za maendeleo, watu-wenye-ualbino wamekuwa na ni miongoni mwa wale "walioachwa nyuma zaidi." Kwahivyo, zinafaa kulengwa kwa mwingiliano kati wa haki za binadamu kwa njia inayotarajiwa na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Kwasababu ya ukosefu wa melanini kwenye ngozi na macho, watu-wenye-ualbino maranyingi wana ulemavu wa kudumu wa kuona. Pia wanakabiliwa na ubaguzi kutokana na rangi ya ngozi zao; kwa hivyo, maranyingi wanakabiliwa na ubaguzi wa aina nyingi na wa kuingiliana kwa misingi ya ulemavu na rangi.

Ingawa watu wenye ualbino wanaishi katika jamii zetu,wengi wetu hatuna kabisa au tuna taarifa kidogo kuhusiana na hali hIyo.”Kukosekana kwa taarifa sahihi kuhusu ualbino”katika mahojiano kadhaa na vyombo vya habari na mikutano ya aina hiyo,Mtaalamu wa kujitegemea kuhusu masuala ya Ualbino wa Umoja wa Mataifa IKPONWOSA ERO,alisema “Changamoto ya kutokuelewa kuhusu hali ya ualbino haipo tu katika nchi zinazoendelea bali pia katika nchi zilizoendelea, hivyo ukiijumuisha upungufu huu kwa mtizamo wa umasikini,imani za kishirikina na sababu nyingine za kiuchumi unapata mchananyiko hatari sana.”Matokeo yake watu wenye ualbino wananyanyapaliwa na mara nyingine wanafanyiwa vitendo vibaya vya ubaguzi katika jamii zao.

• Watu-wenye-ualbino hawapewi majina mazuri katika jamii zetu.Jina maarufu kama “ZERUZERU” ambalo linatafsiriwa kama ‘kiumbe mfano wa mzuka mweupe’.Kwa kanda ya ziwa wasukuma mtu mwenye hali hiyo anaitwa ‘’Mbulimwelu’’ wakimaanisha mbuzi mweupe.Ukerewe wanamuita mtu mwenye ualbino “Embalamwela”wakimaanisha mbwa mweupe.MAJINA KAMA HAYO YANAUDHALILISHA UTU WA BINADAMU WENYE UALBINO.Nchini Nigeria ,watu wa kabila la Hausa wanamuita mtu mwenye ualbino ni ‘Baturebanza’ wakimaanisha ‘mzungufeki’.Wazulu wanamuita mtu mwenye ualbino “Inkawu’kama sokwemtu au Nyani.

• Katika baadhi ya jamii inaaminika kuwa mtoto mwenye ualbino anazaliwa kwasababu mama alipata ujauzito wakati wa kipindi chake cha hedhi.Wengine wanaamini kwamba alifanya ngono au kubakwa na mizuka.Imanii hizo zinasababisha kuvunjika kwa ndoa ,kutengwa n ahata kutelekezwa kwa Watoto wenye ualbino na hivyo Watoto hao hulelewa na akina mama pekee au hupelekwa kwa bibi.

• Baadhi ya watu wameambiwa na waganga wa kienyeji kuwa viungo vya watu wenye ualbino,damu na nywele zao vinapochanganywa na dawa nyingine za kiuchawi vinaweza kumfanya mtu atajirike au apate mafanikio.Imani hii imesababisha mauaji mengi ya watu wenye ualbino,kukatwa viungo ,na hata kutekwa kwao nchini .Wengi wao sasa wanaishi katika maeneo maalumu yaliyotengwa na serikali kwa usalama wao.
Ni dhahiri kwamba mtu anaweza kupata utajiri ,mafanikio na hata kushinda uchaguzi kwa kufanya kazi kwa bidii na siyo vinginevyo.

Ubaguzi kwa watu-wenye -ualbino umeendelea katika jamii licha ya Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya-jamuhuri-ya-muungano-wa-Tanzania-ya-mwaka-1977 kusisitiza usawa wa watu wote mbele ya sheria na kuzuia ubaguzi wa aina yoyote ile.

 Kuhusiana na haki-ya-kuishi inasisitizwa kuimarisha ulinzi wa watu-wenye-ualbino kwa kuzuia aina zote za uhalifu na mashambulizi dhidi yao

 Kutoa bure huduma za utambuzi na matibabu ya saratani ya Ngozi kwa watu-wenye-ualbino ikiwa ni Pamoja na kupatiwa vipeperushi na mafuta-kinga na kurasimisha sare za shule za wanafunzi wenye ualbino kuwa ni mavazi-kinga.

 Serikali kutenga mafungu maalumu kugharamia mpango wa elimu kwa umma na kutengeneza kiwanda maalumu nchini cha mafuta-kinga yanayoendana na mazingira ya mtanzania,kofia za kuzuia jua na visaidizi vya kuimarisha uoni.

 Mwongozo kwa walimu, watoa-huduma za kielimu na wazazi wa watu-wenye-ualbino uchapishwe kwa wingi, usambazwe kwa shule zote na uwe rejea muhimu kwao katika ufundishaji na malezi ili kurahisisha malezi ya watu-wenye-ualbino shuleni na majumbani.

 Kuimarisha hatua za kuhakikisha kuwa watu-wenye-ualbino wanalindwa ikiwa ni Pamoja na kuharakisha uchunguzi wa uhalifu dhidi yao na mashauri ya mahakamani na pia kupambana na tabia ya kuepuka mkono wa sheria na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi za mahakamani kwa kushirikiana na vyombo vya kusimamia sheria..

 Kuanzisha mfumo wa kumlinda mtoa Ushahidi;kutoa bure msaada wa kisheria na ushauri nasaha kwa waathirika wa vitendo vya ukatili ,familia zao na mashahidi wa uhalifu


TIBA YA SARATANI YA NGOZI
Utambuzi wa mapema na tiba sahihi ya saratani ya Ngozi ni changamoto kubwa hapa nchini. Kuna uhaba mkubwa wa madaktari bobezi wa saratani ya Ngozi za watu wenye ualbino na uhaba au ukosefu wa tiba mionzi na vifaa vyake (cryotherapy,liquid nitrogen ,cylinders na cryo guns)) hali inayopelekea upotevu mkubwa wa Maisha ya watu.

Huduma za utambuzi wa mapema haziwezi kuwafikia wahitaji nchi nzima.Hii nii kwasababu kuna hospitali chache za rufaa zinazotoa tiba ya saratani.Hospitali hizo ni (KCMC) Kilimanjaro Christian Medical Center ,Kitengo cha RDTC Moshi,Ocean Road Cancer Institute ya Dar es salaam na Hospitali ya Bugando ya Mwanza.

BeautyPlus_20230608201016716_save.jpg
 
Hawa watu wenye ualbino ni waathirika wakubwa wa magonjwa ya saratani na Tanzania haijawa tayari kutengeneza kiwanda kikubwa cha mafuta yao kusudi wasisumbuke na wasiishiwe.. ipo haja kuwaangalia hawa watu,wengi wao ni wahanga wa ugonjwa wa afya ya akili..
 
Back
Top Bottom