Kigoma mjini mpya

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
SIKU TUKIKUBALI KUBADILIKA KIGOMA MJINI ITABADILIKA.

Kwa tulio wafuatiliaji wazuri wa siasa za Kigoma mjini haswa baada ya kuasisiwa mfumo wa vyama vingi lazima tutakubaliana watu wa Kigoma mjini tumeamua kuwa makabwitunge wa wanasiasa Uchwara wanaojivua majukumu ya uwakilishi na kujivika majukumu ya kupambana na serikali.

Rejea Kaborou alipowageuka na kuwaambia hata msipomchagua chungu chake hakiingii maharage hapo ni baada ya miaka saba ya kumuamini na kujitoa muhanga kumpigania haswa.

Alichofanya Kaborou 2005 Kigoma mjini ndicho alichofanya Zitto Kigoma Kaskazini 2015 tofauti yao mmoja alikimbia jimbo mwingine akabaki jimboni kwake hadi umauti unamfika.

Anachofanya Zitto leo kwa wanakigoma Mjini ni uhuni ambao haustahili kufumbiwa macho au kukaliwa kimya.

Ametugawa wanajimbo kiasi kwamba tunashindwa hata kuhoji aliyotuahidi ametekeleza kwa kiwango gani, anatujaza ujinga wa kujadili sijui katishiwa maisha mara tumjadili Tito Magoti wakati biashara, uvuvi na Kilimo vinakufa jimboni kwake.

Zitto anajitahidi kutengeneza Cinema uchwara ili kututoa katika mjadala wa manispaa inayoongozwa na Chama chake kupata hati chafu tangu iingie madarakani tofauti kabisa na zilizopita.

Leo anafanya siasa za kudanganya watu kawasha taa za barabarani aliozizima yeye na kabwitunge zake the so called madiwani kwa kupiga pesa ziluzotengwa kwa ajili ya uendeshaji wa taa hizo.

Huyuhuyu anayejinasibu mzalendo kwetu watu wa Kigoma mjini kwa kushirikiana na madiwani wake wakaamua kupitisha kodi kandamizi kwa waendesha bajaji ambazo hazipo Popote Tanzania hii.

Zitto anapata kiburi cha kufanya yote haya sababu watu wa Kigoma tumegoma kubadilika na kuendelea kuchukulia siasa kama ushabiki wa mpira badala ya njia ya maendeleo.

Vijana, unakuaje kijana kwa kuamini tuu eti Zitto ndio baba wa Kigoma wakati ukiulizwa kafanya nini tangu achaguliwe unakosa jibu unaishia kumwaga mitusi?

Ni sisi vijana tunaotakiwa kubadilika october hii, tusikubali kuwa daraja la kujenga wanasiasa wachache wanaoichokoza serikali kisha kukimbilia Marekani eti wagonjwa.

Najua, akirudi atawaletea tuu mrejesho wa anatishiwa maisha, atajiita kijana wenu na kuwavimbisha kichwa kwa kuwaita mashujaa na wanamapinduzi msiotingishwa huku yeye akiwatingisha kama mazezeta.

Suluhisho ni moja tuu, kwa sauti moja tuanze kumuuliza ndani ya miaka minne ametuwakilishaje, kashirikianaje na serikali kuhakikisha changamoto zetu zinatatuliwa. Mengine tofauti akaongee na mkewe chumbani.

#NimekubaliKubadilika
#NaipendaKigomaYangu
#KataaUjinga
#OctoberYaKibabe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa ni mbaya sana. Maisha yako yote unaishi Mwanza kwa kutengeneza miziki ya rege halafu unawaambia watu wa Kigoma ujinga huu. Pili nahisi umerudia kuanza kuvuta bangi tena. Jitahidi kwanz kuhudumia familia yako. Saidia kwanza watoto wako waache kuokota chuma chakavu
 
Back
Top Bottom