Kafulila: Tanzania kwa mara ya kwanza tunajenga barabara za kisiasa za kulipia 150km kutoka Kibaha Pwani-Morogoro bila Fedha ya Serikali

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,503
1,118
Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Tanzania Mhe David Kafulila amesema ule mradi wa barabara za kulipia(toll road) uliokwama tangu awamu zilizopita Sasa kwenye awamu hii ya sita umeiva.

Mhe Kafulila amesema, mradi huu utatumia zaidi ya US$ 800 milioni karibu sawa na TZS 2.08Trilioni.

Mhe Mkurugenzi Kafulila amesema barabara zinazokwenda kujengwa zitakuwa ndio barabara Bora zaidi hapa nchi zitakazoishi mpaka miaka 35 bila kufanyiwa Ukarabati mkubwa.

Aidha, Mhe Kafulila amesema nia ni kupunguza msongamano wa magari na watu kati ya Dar-Morogoro-Dodoma ambapo Sasa yule anayehitaji kwenda kwa kasi itamlazimu alipie kiasi Fulani Cha pesa ili apite barabara ya Express.

Mhe Kafulila anaeleza kuwa Tanzania itafunga mkataba na mwekezaji huyo na baada ya mkataba kuisha barabara zitasalia kuwa mali za watoto wa Tanzania.

Kafulila anasema nia kubwa ya Serikali ya Dkt Samia Suluhu ni Watanzania kupata huduma bora kwa gharama nafuu pasina kutumia Fedha ya Serikali.

===​
 
Kweli hii awamu ya mzanzibari imefilisika kimawazo.pesa zote alizokopa,Kodi tunazokamuliwa,misaada na zinginezo ambazo zingejenga barabara ya njia sita kutoka dar Hadi kigoma wao wanatuletea takataka ya kulipia?.yaani Ninunue gari yangu Kodi nakatawa,mafuta Kodi nakatawa,na barabara Tena duh!
 
Kama huwezi kulipia utapita njia ya umma
 
View attachment 2985383
Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Tanzania Mhe David Kafulila amesema ule mradi wa barabara za kulipia(toll road) uliokwama tangu awamu zilizopita Sasa kwenye awamu hii ya sita umeiva.

Mhe Kafulila amesema, mradi huu utatumia zaidi ya US$ 800 milioni karibu sawa na TZS 2.08Trilioni.

Mhe Mkurugenzi Kafulila amesema barabara zinazokwenda kujengwa zitakuwa ndio barabara Bora zaidi hapa nchi zitakazoishi mpaka miaka 35 bila kufanyiwa Ukarabati mkubwa.

Aidha, Mhe Kafulila amesema nia ni kupunguza msongamano wa magari na watu kati ya Dar-Morogoro-Dodoma ambapo Sasa yule anayehitaji kwenda kwa kasi itamlazimu alipie kiasi Fulani Cha pesa ili apite barabara ya Express.

Mhe Kafulila anaeleza kuwa Tanzania itafunga mkataba na mwekezaji huyo na baada ya mkataba kuisha barabara zitasalia kuwa mali za watoto wa Tanzania.

Kafulila anasema nia kubwa ya Serikali ya Dkt Samia Suluhu ni Watanzania kupata huduma bora kwa gharama nafuu pasina kutumia Fedha ya Serikali.

===​
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki sana Rais Samia
 
Express, hapo Nairobi ilianza kujengwa 2021, iantumika siku nyiiiiingi; sina hakika kama na wenyewe wameuza au wamepangisha!

Lifespan miaka 35, anasema mwekezaji akiondoka inabaki kuwa mali ya TZN?
  • Lini TZN iliingia mkataba mdogo kiasi cha kutegemea kabla ya miaka 35 utakuwa umeisha?
  • M/City, ile miaka 100, ishapita mingapi mpaka sasa?

Daraja la kigamboni, na penyewe si tunalipia?
  • Kwakuwa ni fedha za wafanyakazi, mpaka sasa imeingiza kiasi gani?
  • Lini itakuwa mwisho wa kulipia?
-Deni linatarajiwa kulipika lini?
 
Hatulipi deni ila mjenzi ataendesha mradi kwa kipindi Fulani then anatupisha
 
Hawa watu wanachelewa Sana kufikiri nawakifikiri wanajiona magenius balaa.

Inanikumbusha wahuni Manazi na zile ndege zao Luftwaffe's angani na U-boats baharini walivyosumbua dunia.
 
Back
Top Bottom