Je, wajua, kuzimu ni Mtu, na Mauti ni Mtu?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,867
23,764
Salaam, shalom,

Tuendelee na MADA zamivu katika masuala yasiyoonekana Kwa macho.

Usilolijua, sasa tunaishi wakati ambao MUHURI wa nne umekwisha Funguliwa, kuzimu imeruhusiwa kuja Duniani kuvuna Roho za wakaao duniani theluthi Moja,

Unashangaa Bado watu wanaenda kwenye mabaa na kununua Malaya, Kuna maeneo sasa ni kuzimu za Duniani, centers ndogo ndogo za kuzimu, mmekwisha tajiwa Hadi maeneo, kitambaa white ni mojawapo, mnapuuza, tusubiri.

MTU. Mtu ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mwanadamu ana mwili wa nyama, lakini Malaika wa Nuru au Giza wao pia Wana miili ya kiroho.

Kwa tafsiri hiyo, mwanadamu ni mtu, Malaika wa Nuru ni mtu, Malaika wa Giza ni mtu, na Malaika wa Nuru ni mtu vile vile. Ardhi ni mtu, Ina kinywa, Ina sikio, Ina mdomo, moyo ( moyo wa Nchi)nk nk

Kuzimu Ina tafsiri mara mbili, kuzimu ni gereza lililofungwa, Lina mlango/ mfuniko sababu ni shimo. Kuzimu Ina Tumbo linalomeza waingiapo humo, ndani Pana funza na minyororo ya moto uwakao nk nk

TAFSIRI ya pili ,

Kuzimu ni MTU, shimo la KUZIMU ni MTU vile vile, waulize wote waliowahi kufa wakarejea watakwambia, wengine utawasikia wakisema, Malaika wa kifo amemchukua , wengine husema mtoa Roho kampitia nknk.

MAUTI vile vile ni mtu, Kwa kuwa ana umbo ,NAFSI na Roho, ndivyo vilivyo viumbe vya kiroho.

Maji pia ni mtu, Kwa kuwa ana uhai, maji Yana Roho, NAFSI na mwili.

MADA: MAUTI NA KUZIMU NI MTU KIVIPI?

Ili mtu uhai umtoke, lazima waje wahusika wa kuvuna Roho, Ukiwa ni WA Ibilisi, atakuja huyo MAUTI akifuatana na askari wake, Akiwa wa Mungu, pia atafutatana na Malaika wake.

KUFUNGULIWA KWA MUHURI WA NNE. (UFUNUO 6:8)

NIKAONA NA TAZAMA FARASI WA RANGI YA KIJIVUJIVU,NA YEYE ALIYEMPANDA JINA LAKE NI MAUTI, NA KUZIMU AKAFUATANA NAYE. NAO WAKAPEWA MAMLAKA JUU YA ROBO YA NCHI,WAUE KWA UPANGA NA KWA NJAA NA KWA TAUNI, NA KWA HAYAWANI WA NCHI.

Utaona hapo juu MAUTI Huwa anafuatana na kuzimu, hiyo ni HALISI. USALAMA ni kuwa ndani ya Yesu, kuishi maisha matakatifu.

MUHURI wa 4 umefunguliwa 2020 July, KUFUNGULIWA Kwa MUHURI huo ndio kulikuja na ugonjwa Toka kuzimu wa CORONA, Nia ni kuua, na sababu ya maombi ya WATAKATIFU Kwa namna Fulani, target ya vifo haikufikiwa,

Vita umeviona vinaendelea duniani kote, njaa yaja Dunia nzima,Matetemeko, mdororo wa Uchumi, magonjwa nk nk

Kuanzia 2026, patakuwa na njaa Dunia nzima, ukame mkali, jua litakuwa adjusted na kushushwa chini kidogo, shida hiyo itadumu Kwa miaka 3 na nusu, so many will die.

Yanakuja matetemeko na majanga ya Kila aina,MAPINDUZI, nknk Ili kutimiza Ruhusa iliyotolewa na Mungu WANADAMU wafe.

Watu watakufa Hasa wanaokataa kumcha Mungu, watenda dhambi, maana mtakatifu akifa hakuna HASARA, Yeye ni raia wa Mbinguni, HASARA ni Kwa asiyeokoka.

Nakusihi Kwa Jina la Mungu, Muda waRehema na kuvumilia watenda dhambi umeisha, muda umeisha Wana wa Mungu, mgeukieni Mungu.

Ikiwa unapenda kumrudia Mungu, fuatisha Sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN.
 
(Yohana 1:5)
Nayo Nuru yangaa gizani Wala Giza halikuiweza.

Giza litashindana nami, lakini halitaniweza, maana kuitaja kuzimu na MAUTI wanasikia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom