Je ni albam gani ya wasanii wa hiphop Tanzania uliisikiliza na kuiona ni albam bora na siyo bora albam??

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,382
12,950
hizi ndiyo albam zangu bora kabisa za hiphop zilizofanywa na wasanii wa Tanzania

(1) PROF JAY, albam yake inayoitwa MACHOZI, DAMU NA JASHO hii albamu huwa siichoki kuisikiliza ina kila kitu elimu,kufurahisha na kusisimua jamii mwamba ukimsikiliza katika hii albamu unajua kabisa he is a geneus uandishi floo ni hatari sana.

(2)MWANA FA, album inaitwa MWANAFALSAFANI kipindi hicho mwili mdogo ila akili kubwa lugha majigambo na floo humu naibu waziri wa Sanaa kwa sasa alitisha sana ni moja kati ya albamu bora kabisa huwa naisikiliza mpaka sasa na huwa sichoki kuisikiliza kabisa humu kuna mawe ya kutisha

(3) NIKKI MBISHI ,albamu yake ya SAUTI YA JOGOO kipindi nakua nilikua nina ndoto ya kuwa msanii lakini nilipokuja kumsikia huyu mwamba niliona bora nibaki kuwa shabiki nilichana daftari langu la vesi nikki humu kaimba kila kitu siasa za roma zimejaa humu katika hii albam kizazi cha nikki ndiyo kizazi kilicholeta punch line, floo kali zilizojaa elimu ndani yake hakika nikki kaja ubadili hali ya hewa ya hiphop

(4) FID Q Albamu ya VINA MWANZO KATI NA MWISHO, kupitia albam hii uwa naona fid kafanya kazi kubwa sana katiaka mziki huu wa bongo humu yamejaa mawe ya kutosha ngosha anaandika vizuri sana ukimfuatilia nyimbo zake zinaelimisha sana
mfano kuna mstari anasema ''chipukizi chapeni kazi ili mng'atuke na mlipo kwama….//
vumilieni kama nyota kutoka jua likizama…//

hii ngoma inaitwa ripoti za mitaaani ft prof jay na langa Tanzania hii hakuna kama fid kwa uandishi hilo halina ubishi

(5)ONE THE INCREDIBLE albam yake inaitwa SOGA ZA MZAWA Kudadadekii ni moja kati ya albam bora kabisa katika playstore yangu humu kuna vyuma kama mtumwa, soga za mzawa mtumwa inaelezea Maisha halisi ya mtu mwenye kipato kidogo anayeyumbishwa na wanasiasa na ndiyo Maisha tuliyonayo kwa sasa thamani ya mpiga kura haithaminiwi na viongozi ambao aliwapigia kula

(6) STEREO albamu inaitwa THE AFRICAN SON , dogo alimwaga nondo sana humu elimu yake kaitumia vizuri sana katika kufundisha jamii punchline na flow kali hapa ndiyo mahala pake kuna nyimbo inaitwa afande Nyati ,Swahili chundabadi mjahidina ,nitabaki juu, nk humu kawachezea sana marapa kawageuza kama mishikaki kwa upangaji wake vina na floo kali

hizo ndizo albam zangu bora za muda wote je wewe unazozipi share nasi ili na sisi tukasikilize albam yako bora ya wasanii kutoka Tanzania??
 
Dizasta vina
A father figure AFF
huyu mwamba toka afanye tribulation kwa dogo yule wa bongo record alimuua mazima kabisa huyu ni moja kati ya marapa wanakuja wanaandika sana dizazista weka mbali na watoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom