Hii ndiyo maana ya "Unbeaten record"

wadzelino

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
205
316
Hebu ona hii
  • Tumewekeza kuliko Al Hilal.
  • Manara kaja na siri ya ushindi wa Simba.
  • Raha yetu kuwafunga Simba.
  • Nabi: Mechi za kirafiki za kimataifa kwetu hazina kipaumbele.

Tathmini:
Mwenye akili timamu kati ya hao yupo kweli?

Je, kitaalamu hiyo timu inaendeshwa kwa mfumo rasmi au inaendeshwa kiholela?

Niwapongeze Simba kwa kuwa mmepiga hatua katika mpira, kwani hata mpitie changamoto zote pamoja na kejeli za wale, hata wawafunge mara 4 huchukulia kama hao ni timu ndogo ambayo lazima iikamie timu kubwa.

Kwa yanga hawako makini, wamefanya mpira kama siasa, na kocha mtaalamu anakataa mechi za kujipima za kimataifa kisa kudumisha rekodi ya kutokupigwa. Ama hakika wenye akili ni wawili tu pale, wengine wote kama alivyosema Luc, akiwemo wa kupigwa ban.

Mwisho: Mechi bado iko wazi, nendeni mkapambane Sudan, japo kisaikolojia kuhimili figisu zao nje ya uwanja kwa sisi wabongo ni mtihani.

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Tunaweka kumbukumbu

311436467_1998460140359514_3503576000815617817_n.jpg
 
Back
Top Bottom