FIFA wanaua soka, Kila timu inayoshiriki kombe la dunia la vilabu kupewa takribani shilingi bilioni 130, Mpira wa Afrika unaenda kuwa farmers league

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
275
800
Hasa hapa kwetu Afrika kwenye timu ambazo hazifiki hata asilimia kumi ya hicho kiasi

Unazipa timu bilioni 130 kwa kushiriki kombe la mwezi, inakuwa ngumu sana kwa timu zenye bajeti za bilioni 8 kushindana na hao wanaopewa mizigo mizito.

Vuta Picha leo hii hata Mtibwa kavuta hicho kiasi, Yanga na Simba wataweza kumsogolea ?
 
Hasa hapa kwetu Afrika kwenye timu ambazo hazifiki hata asilimia kumi ya hicho kiasi

Unazipa timu bilioni 130 kwa kushiriki kombe la mwezi, inakuwa ngumu sana kwa timu zenye bajeti za bilioni 8 kushindana na hao wanaopewa mizigo mizito.

Vuta Picha leo hii Yanga au Simba kavuta hicho kiasi, kuna shindani tena hapo ?
Ndiyo maana kila njia ilifanyika ili goli la Aziz Ki lisikubaliwe ili Mamemlodi waingine kwenye bwawa hilo la mihela ya FIFA.
 
Kama refa alikuwa amepanga kuwabeba Mamelodi angewapa penalti kwa Mamelodi, Memelodi wenyewe wamefungwa na Esperance goli lenye utata wa offside, kama kuna njama za kuwabeba hilo goli lingekataliwa..Alijitahidi kuwa fair ila mistakes huwa zinatokea
 
Hasa hapa kwetu Afrika kwenye timu ambazo hazifiki hata asilimia kumi ya hicho kiasi

Unazipa timu bilioni 130 kwa kushiriki kombe la mwezi, inakuwa ngumu sana kwa timu zenye bajeti za bilioni 8 kushindana na hao wanaopewa mizigo mizito.

Vuta Picha leo hii Yanga au Simba kavuta hicho kiasi, kuna shindani tena hapo?
bajeti ya ahly ni dola milion 100+ kwa mwaka!

hizo dola mil 50 wala haziwafanyi wao kuwa bora zaidi kutuzidi,

afrika hii timu zijitahidi kufanya scouting, wachezaji wazuri ni wengi sana!

simba na yanga ingekua zinajiendesha kisasa zina uwezo wa kutengeneza mapato zaidi ya 20b kwa mwaka, kiasi ambacho kinatosha kuendesha timu na ikawa na ushindani........

1. kadi za wanachama
2. bidhaa za timu (jezi, skafu, kalenda, kanga, makoti, vyombo vya vyakula vyenye logo zao, etc...... hapa ndio pana pesa ndefu zaidi)
3. gate collection (hapa wanatakiwa kukodisha uwanja, ila wavune vizuri mapato through corporates, migahawa, viingilio, majukwaa unayauza kwa makampuni yajitangaze n.k)
4. media
5. ...
6....
7....

katika nchi kama hii ambayo wapenda mpira ni wengi, ni rahisi sana kuwageuza pesa!
 
So far

Naona Azam na Yanga wanapambana kutumia hiyo mianya walau ila bado saaanaa
Sijui Kwa Simba nao
 
Kama refa alikuwa amepanga kuwabeba Mamelodi angewapa penalti kwa Mamelodi, Memelodi wenyewe wamefungwa na Esperance goli lenye utata wa offside, kama kuna njama za kuwabeba hilo goli lingekataliwa..Alijitahidi kuwa fair ila mistakes huwa zinatokea

Weka evidence kama mamelodi amefungwa goli la offside na Esperence

Weka ushahidi. Kuprove hoja yako
 
Kama refa alikuwa amepanga kuwabeba Mamelodi angewapa penalti kwa Mamelodi, Memelodi wenyewe wamefungwa na Esperance goli lenye utata wa offside, kama kuna njama za kuwabeba hilo goli lingekataliwa..Alijitahidi kuwa fair ila mistakes huwa zinatokea
Una makengeza wewe lile goli lina utata gani?
 
Kama Goli la esperence lingekuwa na utata mbona VAR na wala hakuna Debate yoyote ya kulichambua kama lina utata ?

Goli la yanga liliongelewa kila sehemu kuanzia kwenye mitandao mpaka kwenye media kubwa
 
Kama refa alikuwa amepanga kuwabeba Mamelodi angewapa penalti kwa Mamelodi, Memelodi wenyewe wamefungwa na Esperance goli lenye utata wa offside, kama kuna njama za kuwabeba hilo goli lingekataliwa..Alijitahidi kuwa fair ila mistakes huwa zinatokea
Aziz Ki hakufunga goli likakataliwa? Jitihada zilifanyika swali Lomalisa spate red card aibu ukala kubwa
 
Hasa hapa kwetu Afrika kwenye timu ambazo hazifiki hata asilimia kumi ya hicho kiasi

Unazipa timu bilioni 130 kwa kushiriki kombe la mwezi, inakuwa ngumu sana kwa timu zenye bajeti za bilioni 8 kushindana na hao wanaopewa mizigo mizito.

Vuta Picha leo hii Yanga au Simba kavuta hicho kiasi, kuna ushindani tena hapo?
Yeah!...mpira wa Sasa umevamiwa na mabwanyenye..

Usisahau FIFA ni shirika la Kibepari linalotafuta faida.
 
Kwa Africa Ni timu 4 tu zinaenda zilizofanya vizuri ndani ya miaka mitano,

Simba hayumo lakini anashika namba 7 kashaingia robo fainali mara nyingi miaka mitano iliyopita,

Yanga yupo nje ya top 10 kaanza kupata mafanikio mwaka jana
Bingwa wa CAF champions league ana tiketi ya moja kwa moja bila kujali ranks.. yule refa alitufanyia umafia sana kule south afrika, timu zilizobaki semis zote tunazimudu, tulikua tunaenda kukipiga na wakina man city.
 
Mamelodi analazimishwa afike mbali sababu yeye peke yake ndie anategemea ranking.

1.AL AHLY ameshafuzu sababu ndani ya misimu mitano iliyopita amebeba ligi ya mabingwa mara 2.

2.Waydad ameshafuzu sababu ndani ya misimu mitano iliyopita amebeba kombe la klabu bingwa mara moja

3. Esperence ameshafuzu sababu ndani ya misimu mitano iliyopita amebeba kombe la klabu bingwa mara mbili.

4. Nafasi ya nne ndio bado tupu. Maana ni only 3 teams ndizo zilizobeba ubingwa wa africa last 5 years.

Na hiyo nafasi ndio itapewa klabu ambayo itakuwa na ranking ya juu. Kama hatatokea bingwa mpya. Mfano yanga tungeenda fainali na kutwaa ubingwa hiyo nafasi tungepewa sisi.

Tp mazembe akienda fainali na kutwaa ubingwa hiyo nafasi anapewa yeye

Na hata mamelodi kama akitwaa ubingwa anapewa yeye.

Kama mamelodi ataukosa ubingwa na tp mazembe nae ataukosa ubingwa basi mamelodi atapewa hiyo nafasi ya nne ya kushirikiki kwa kigezo cha ranking ya juu.
 
Back
Top Bottom