Elimu ya bure kwa mnaojiuliza Bendi za Congo DR zinapata wapi pesa za kujiendesha pamoja na wamiliki wake kuwa matajiri

1. Hakuna Msaniii yoyote mkubwa wa Congo DR kuanzia kwa JB Mpiana, Koffi Olomide, Werrason, Felix Wazekwa, Roga Roga na Bendi yake ya Extra Musica, Fally Ipupa na Ferre Gola utamuita aje nchini Kwako kufanya Show bila ya Kwanza kumuingizia katika Akaunti yake kuanzia Shilingi Milioni 400 hadi 500 za Kitanzania.

2. Malipo yao pia hutegemea na nchi ambayo wanaenda Kufanya Shows zao. Kwa mfano wakiwa wanaenda nchi za Ulaya na hata Marekani huko ambako pia Waafrika wanaopenda Nyimbo zao/Miziki yao Gharama zao ambazo huwa wanataka wapewe Kwanza ndiyo waelekee huko huanzia kati ya Shilingi Milioni 800 za Kitanzania hadi Shilingi Bilioni Moja.

3. Mwisho kabisa Chanzo chao Kikubwa cha Mapato ni Ubunifu wao wa Kutoza Pesa kwa kila Mtu ambaye anafagiliwa katika Wimbo mpya na wa Album mpya. Kiasili Wakongo ni Watu ambao wanapenda Sifa, Kujulikana na Ufahari kiasi kwamba hata Watani zangu Wahaya na Ndugu zangu Wajita kutoka Mkoa wa Mara wanasubiri (namaanisha hawafui Dafu) Kwao.

Zifuatazo ni Gharama (Tozo) kwa Mtu yoyote (hata Wewe Mtanzania Mwenzangu) ukitaka ni ruhksa za Kuchajiwa kama tu utataka Jina lako au Biashara yako litajwe/itajwe katika Wimbo mpya wa hawa Wasanii Tajwa hapa.

- Ukitaka Jina lako litajwe mwanzoni mwa Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 100000

- Jina lako likitajwa katikati ya Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 7500

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene linaanza utalipa Dola za Kimarekani 5000

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene sasa limeshakole utalipa Dola za Kimarekani 3000

- Jina lako likitajwa pale Muziki ukiwa unaenda Kuisha (na huku ndiko Wengi hupataka) basi utalipa Dola za Kimarekani 2000

Na hakuna Nyimbo zozote za Wasanii hawa Tajwa (hasa zile Mpya) mnazozisikia hakuna Majina yasiyopungua 50 hadi 70 huyasikii yakitajwa humo hivyo.

Wewe kaa chini sasa hapo ulipo na upige Hesabu ni kiasi gani cha Pesa hawa Wanamuziki huwa wanakiingiza na ambacho ndicho huwa kinawapa Jeuri ya Kuvaa Nguo za Thamani Kubwa, Kuendesha Magari ya Kifahari, kuwa na Makazi Ulaya (hasa Ufaransa na Ubelgiji) na kuwa na Mahekalu huko Kwao Congo DR hasa katika Mji ambao Masikini hawezi Kuuishi wa Kinshasa kutokana na kuwa ni Mji wenye Gharama kubwa.

Mishahara ya Waimbaji wao wote ambao huwa mnawaona Stejini (hasi wale Marapa ambao Kwao huitwa Atalakus na Kifaransa wanaitwa Animateurs) huwa ni Shilingi Milioni Saba za Kitanzania huku wale Wadada Wanaenguaji ambao huwa mnawaona na baadhi yenu Kuwaona kama vile huwa Wanajidhalilisha huwa wanalipwa kila Mmoja Mshahara wa Shilingi Milioni Tano za Kitanzania kwa kila Mwezi.

Mwisho kabisa kinachoendelea kuwapa Jeuri hawa Wasanii tajwa na Bendi zao ni Udhamini mbalimbali ambao wanaupata kutoka katika Makampuni makubwa ya Vinywaji kama Primus na ile ya Simu ya MTN bila kusahau na Kampuni zingine Kubwa za Mavazi na Mitindo zilizoko Ulaya (Marekani, Ufaransa na Ubelgiji)

Haya na Mimi GENTAMYCINE bado najichanganga hapa tararibu ili angalau nipate tu Dola zangu 2000 ili nimtafute JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge Musica BCBG wanitaje mwishoni mwa Wimbo kwa Majina yangu halisi ya Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura ambayo hata Marafiki zangu wakubwa hapa akina adriz, Bujibuji Simba Nyamaume na King Kong III wanayajua vyema ili nikitajwa nae nije niwakoge (niwatambie) hapa hadi mkome.
Kajanja
 
kuna interview moja niliwahi iona jb mpiana anahojiwa akiwa kwake, aisee ile sio nyumba bali jamaa anaishi hotelini tena 5 star, kamera ikapelekwa parking, aisee yale magari anayomiliki sio mchezo, siku baada ya kuiangalia ile interview nikaja kutana na ali choki wa twanga pepeta sehemu na usafiri wake nilijikuta nacheka kwa nguvu😂
 
ila mkuu hapo kwa dancers kulipwa million 5 kwa mwezi nakataa, ingekuwa hivyo wasingekuwa wanazamia nchi za ulaya na marekani pindi bendi zinapoenda huko kupiga show
 
Mamaaa
1. Hakuna Msaniii yoyote mkubwa wa Congo DR kuanzia kwa JB Mpiana, Koffi Olomide, Werrason, Felix Wazekwa, Roga Roga na Bendi yake ya Extra Musica, Fally Ipupa na Ferre Gola utamuita aje nchini Kwako kufanya Show bila ya Kwanza kumuingizia katika Akaunti yake kuanzia Shilingi Milioni 400 hadi 500 za Kitanzania.

2. Malipo yao pia hutegemea na nchi ambayo wanaenda Kufanya Shows zao. Kwa mfano wakiwa wanaenda nchi za Ulaya na hata Marekani huko ambako pia Waafrika wanaopenda Nyimbo zao/Miziki yao Gharama zao ambazo huwa wanataka wapewe Kwanza ndiyo waelekee huko huanzia kati ya Shilingi Milioni 800 za Kitanzania hadi Shilingi Bilioni Moja.

3. Mwisho kabisa Chanzo chao Kikubwa cha Mapato ni Ubunifu wao wa Kutoza Pesa kwa kila Mtu ambaye anafagiliwa katika Wimbo mpya na wa Album mpya. Kiasili Wakongo ni Watu ambao wanapenda Sifa, Kujulikana na Ufahari kiasi kwamba hata Watani zangu Wahaya na Ndugu zangu Wajita kutoka Mkoa wa Mara wanasubiri (namaanisha hawafui Dafu) Kwao.

Zifuatazo ni Gharama (Tozo) kwa Mtu yoyote (hata Wewe Mtanzania Mwenzangu) ukitaka ni ruhksa za Kuchajiwa kama tu utataka Jina lako au Biashara yako litajwe/itajwe katika Wimbo mpya wa hawa Wasanii Tajwa hapa.

- Ukitaka Jina lako litajwe mwanzoni mwa Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 100000

- Jina lako likitajwa katikati ya Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 7500

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene linaanza utalipa Dola za Kimarekani 5000

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene sasa limeshakole utalipa Dola za Kimarekani 3000

- Jina lako likitajwa pale Muziki ukiwa unaenda Kuisha (na huku ndiko Wengi hupataka) basi utalipa Dola za Kimarekani 2000

Na hakuna Nyimbo zozote za Wasanii hawa Tajwa (hasa zile Mpya) mnazozisikia hakuna Majina yasiyopungua 50 hadi 70 huyasikii yakitajwa humo hivyo.

Wewe kaa chini sasa hapo ulipo na upige Hesabu ni kiasi gani cha Pesa hawa Wanamuziki huwa wanakiingiza na ambacho ndicho huwa kinawapa Jeuri ya Kuvaa Nguo za Thamani Kubwa, Kuendesha Magari ya Kifahari, kuwa na Makazi Ulaya (hasa Ufaransa na Ubelgiji) na kuwa na Mahekalu huko Kwao Congo DR hasa katika Mji ambao Masikini hawezi Kuuishi wa Kinshasa kutokana na kuwa ni Mji wenye Gharama kubwa.

Mishahara ya Waimbaji wao wote ambao huwa mnawaona Stejini (hasi wale Marapa ambao Kwao huitwa Atalakus na Kifaransa wanaitwa Animateurs) huwa ni Shilingi Milioni Saba za Kitanzania huku wale Wadada Wanaenguaji ambao huwa mnawaona na baadhi yenu Kuwaona kama vile huwa Wanajidhalilisha huwa wanalipwa kila Mmoja Mshahara wa Shilingi Milioni Tano za Kitanzania kwa kila Mwezi.

Mwisho kabisa kinachoendelea kuwapa Jeuri hawa Wasanii tajwa na Bendi zao ni Udhamini mbalimbali ambao wanaupata kutoka katika Makampuni makubwa ya Vinywaji kama Primus na ile ya Simu ya MTN bila kusahau na Kampuni zingine Kubwa za Mavazi na Mitindo zilizoko Ulaya (Marekani, Ufaransa na Ubelgiji)

Haya na Mimi GENTAMYCINE bado najichanganga hapa tararibu ili angalau nipate tu Dola zangu 2000 ili nimtafute JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge Musica BCBG wanitaje mwishoni mwa Wimbo kwa Majina yangu halisi ya Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura ambayo hata Marafiki zangu wakubwa hapa akina adriz, Bujibuji Simba Nyamaume na King Kong III wanayajua vyema ili nikitajwa nae nije niwakoge (niwatambie) hapa hadi mkome.
 
kama ni kweli basi koffi pesa anayo maana kuna kipindi alikuwa na waimbaji wote wazuri kwenye bendi yake, safu ilikuwa na waimbaji kama FALLY IPUPA,MONTANA KAMENGA,FERRE GOLA, GIPSON CARNAL BUTAKONDORO,SHELLA MPUTU,GEKO MPELA(mdogo ake Alain mpela),SOLEIR WANGA,SUPER SONIC MILADJI na wengine kibao, kwenye maatalaku nawaokumbuka ni BRIGADE SABARTIN, BEBE KERO(KEROSENE) hao wote ni wakubwa imagine kila mwezi wavute 7 million bado wanenguaji na wapiga vyombo!
 
Back
Top Bottom