Dkt. Biteko aagana na Balozi wa Tanzania nchini Comoro

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
795
504
DKT. BITEKO AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI COMORO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Said Yakub, aliyekwenda kumuaga ofisini kwake leo Mei 9, 2024 Jijini Dodoma.

Dkt. Biteko amempongeza Balozi Yakub kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kuiwakilisha Tanzania katika Visiwa vya Comoro.

Aidha, amemuasa kutumia vyema nafasi hiyo kwa Taifa, hasa kwa kuainisha maeneo ya kimkakati ambayo yatawezesha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za uchumi na maendeleo ya kijamii.

Kwa upande wake Balozi Yakub amemshukuru Naibu Waziri Mkuu na kuahidi kuongeza fursa mbalimbali kwa Watanzania Visiwani humo.

20240509_201303_InSave_1.jpg
20240509_201303_InSave_0.jpg
 
Mie sijuagi anachofanya huyu mtu hata kuanzisha thread kuhusu yeye ni kazi ngumu kuielezea hadi ueleweke kuna watu wanajitahidi kutaka kumpamba hata kwa mgongo wa chupa ila chupa zinagoma kuteleza, ni sawa na hii thred yaani haina hata mvuto kama mhusika mwenyewe.
 
Jambazi Said Yakubu the right hand person wa January Makamba finally katupwa mbali na mirija ya fedha. Huyu mwamba usimuweke jirani na fedha ni hatari kubwa. Akiwa PA wa Ndungai wakati Ndugai kalazwa India alipiga fedha zaidi ya milioni 600 kwa matibabu feki.
 
Back
Top Bottom