Dada apigwa na majirani kwa kumnyanyasa mdogo wake, baba mzazi atoroka eneo la tukio

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,214
4,160
Wanawake wa mtaa wa Iborero Kata ya Nyankumbu mkoani Geita, wamempiga mwanamke mwenzao aitwaye Anastazia Jackson (aliyekaa kwenye picha), kutokana na tabia yake ya kumpiga mara kwa mara na kumchoma moto mdomoni mdogo wake (Wameshea Baba), mwenye umri wa miaka miwili akimtuhumu kudokoa nyama ya kuku iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni.

Wananchi hao wameeleza kuwa tangu watoto hao watatu wafiwe na mama yao mzazi dada yao huyo ambaye ni wa kambo amekuwa akiwatesa watoto hao ikiwemo kuwanyima chakula pamoja na kuwatumikisha kazi ngumu.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Iborero Stephano Samson, pamoja na Kamanda wa Sungusungu wamefika katika familia hiyo na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha polisi huku baba mzazi wa mtoto huyo akitoroka eneo la tukio.

1688932301841.jpeg

 
Dah mtoto mdogo anakuwa na roho mbaya kiasi hicho. Ila Geita kwa matukio iko vizuri mpaka huwa napaogopa.

Ila panaitwa Nyankhumbu sio Nyankumbu.
 
Nayeye wange muunguza moto mdomoni, ili aone uhalisia wa kile alichokua anawafanyia wenzie.
 
Wanawake wa mtaa wa Iborero Kata ya Nyankumbu mkoani Geita, wamempiga mwanamke mwenzao aitwaye Anastazia Jackson (aliyekaa kwenye picha), kutokana na tabia yake ya kumpiga mara kwa mara na kumchoma moto mdomoni
Geita kama Geita tena ndani ya Trend
 
Back
Top Bottom