Ndagullachrles
Member
- Jun 20, 2023
- 71
- 83
Jeshi la polisi nchini limewahakikishia Watanzania Hali ya Amani na usalama wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru utakaofanyika kesho Jumanne mkoani Kilimanjaro.
Tukio Hilo la kuwasha mwenge litafanyika kwenye uwanja wa mpira wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. Mgeni rasmi Katika sherehe hizo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na ni tikio la pili kuwashwa kwa mwenge huo katika mkoa huo baada ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.
Kamishina wa Oparesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini(CP), Awadh Haji amesema Leo mjini Moshi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuimarisha usalama Katika sherehe hizo.
Ameonya kuwa yeyote atakayeonekana kuleta vurugu atashughulikiwa ipasavyo na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya Dola kuwafichua wahalifu.
"Naomba niwahakikishie watanzania sisi jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Dola tumeimarisha ulinzi Katika tukio la kesho"
Pia CP Awadh alisema jeshi la polisi pia litaimarisha Hali ya usalama wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mapema Mwaka huu pamoja na uchaguzi Mkuu hapo mwakani.
Karibuni Moshi mji wa mlima Kilimanjaro tuuwashe Mwenge wa Uhuru pamoja.