CAG: Askari Magereza Walipwe Posho ya Mazingira Magumu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,833
4,586
1713192505592.png

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza Serikali ifanye mapitio ya kina ya mgawanyo wa bajeti kwa ajili ya posho za mazingira magumu kwa Maofisa wa Magereza na kuboesha bajeti kuhakikisha ustawi wa Maofisa wa Magereza.

Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema “Kanuni ya 46(1) ya Kanuni za Utumishi wa Magereza ya Mwaka 1997 inawataka Maofisa Magereza wote wawe na haki ya kupata posho ya mazingira magumu, usafiri, na posho ya kazi za usiku”

“Wakati wa ukaguzi wangu nilibaini kuwa Idara ya Jeshi la Magereza (Fungu 29) ilitenga bajeti ya Sh. bilioni 18.25 kwa ajili ya posho ya mazingira magumu, ambayo ni sawa na asilimia 15 ya mshahara, hata hivyo, katika mwaka wa fedha 2022/23, Maofisa wa Magereza hawakulipwa posho zao za mazingira magumu kutokana na kutopewa fedha kutoka Hazina, kutolipwa kwa posho za mazingira magumu kwa Maofisa wa Magereza kunaweza kuathiri ari ya ufanyaji kazi na ustawi wao”
 
Askari Magereza wanadai kuna wengine wanalipwa hiyo hela ya mazingira magumu na wengine hawalipwi. Hii ikiwa na maana hilo fungu kuna wachache wanakula huko juu
 
CAG amependekeza Kwa Serikali kuanza kuwalipa Askari Magereza posho ya mazingira magumu ya kazi ikiwemo nights pamoja na stahiki zingine.

Kiukweli imenishangaza kwamba Magereza pamoja na kazi Yao ngumu ya kuhangaika na wafungwa harsh nk lakini Serikali ilikuwa haiwajali Kwa kiasi hiki? Huu ni uonezi na sio fair kabisa.

Hawa Magereza na Wenyeviti wa Vijiji/Mitaani ni kada muhimu sana.

My Take
Unakuta wajinga Fulani wanasema Walimu Walipwe posho ya mazingira magumu,unauliza Mwalimu ana mazingira yapi magumu wakati ni mtumishi anafanya kazi siku chache kabisa Kwa mwaka na Wana mishahara mikubwa pia.
 
View: https://www.instagram.com/p/C5ySh_nClJM/?igsh=N2llbHJtNGV6d3py

My Take
Unakuta wajinga Fulani wanasema Walimu Walipwe posho ya mazingira magumu,unauliza Mwalimu ana mazingira yapi magumu wakati ni mtumishi anafanya kazi siku chache kabisa Kwa mwaka na Wana mishahara mikubwa pia.

Kwani Magereza wanafanya kazi masaa mangapi? Endeleeni kuwaona Walimu ni watu wasiofaa ila madhara yake ni ya muda mrefu. Migomo ya kimya kimya ambayo wala mtu hajali, ila bomu lake Kwa Taifa ni kubwa. Acha Watumishi wote wapate motisha wafanye kazi Kwa ari bila kuzingatia kada.
 
Sio tuu masaa mangapi Bali kazi zao Zina call mda wowote,Mwalimu hana hayo mazingira magumu.

Serikali ilikamilisha taratibu za Tume ya walimu na kuanza kuwafanyia usaili hakuna Mwalimu kanjania atapata kazi Ili aje kuganga maisha.

Ambae hawezi atatimuliwa kama sekta zingine wanavyowatimua.
 
Popote askari wa magereza au zimamoto ataonekana anafanya kazi ktk mazingira magumu,basi polisi anatakiwa awe ameishafanyiwa tathimini hiyo kwa thamani ya X2.

Ikumbukwe hata tamko la kutolipa nauli askari liliwarenga polisi,askari wengine waka adopt pia.
Kwa kuzingatia polisi atahangaika sana kutekeleza majukumu,kama atalipa nauli atamaliza mshahara wote huko

Lakini kama kawaida serikali yetu huwa inaendeshwa kwa mood za watu,ndip sababh hata waalimu wana maisha waliyo nayo.
 
Sio tuu masaa mangapi Bali kazi zao Zina call mda wowote,Mwalimu hana hayo mazingira magumu.

Serikali ilikamilisha taratibu za Tume ya walimu na kuanza kuwafanyia usaili hakuna Mwalimu kanjania atapata kazi Ili aje kuganga maisha.

Ambae hawezi atatimuliwa kama sekta zingine wanavyowatimua.
Acha wewe, karibu walimu wote wanafanya kazi hadi muda wa ziada. Usidhani kazi ya mwalimu itakamilika ndani ya muda wa kazi jidanganye wewe. Nchi itaendelea kuzalisha mazombi ngoja niishie hapo.
 
Back
Top Bottom