OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 3,872
- 9,728
Nimeona mdau mmoja humu anahamasisha watu wazame bush wakanunue kwa bei ndogo walete mazao mjini wauze kwa bei kubwa ili wapige pesa.
Hili wazo ni zuri sana lakini ni vyema tupeane tahadhari. Katika biashara zenye umafia mwingi basi hii ya nafaka kwangu ndio namba moja kwa umafia yaliwahi kunikuta.
Nitatoa umafia niliokutana nao ila pia wadau wengine watakuja kuleta ushuhuda.
Miaka flani Niliwahi kuzama bush na milioni moja nikakusanya magunia ya mpunga 20 ya debe 6 yale nkaenda kukoboa kisha nkaweka kwenye fremu yangu lengo niwe nauza kwa bei ya jumla, ule mchele ulitoka vizuri mno changamoto ikawa wali wake ukipikwa hauna ladha, wateja wote wakanikimbia nikaanza kuuza reja reja kwa bei ndogo lakini bado wakanikimbia walikuja mwanzo mwanzo kisha wakaishia mitini.
Baada ya kufanya uchunguzi nikagundua niliuziwa mpunga uliokaa miaka mingi stoo (kumbuka niliununulia bush) pia ile mbegu ya huo mpunga hutoa kilo nyingi lakini wali wake hua hauma radha. Niliuza kwa bei ya hasara mzigo wote kwa wauza vitumbua.
Nkajipanga tena awamu hii nkaamua niende mashineni nikanunur mzigo kwa bei chee kisha niuze kwa bei ya hapo mtaani. Nilinunua kilo 500 kufikisha mzigo kwenye fremu wateja wakafurika nkauza sana hiyo siku. Nashangaa jioni watu wanarudisha mchele wanadai unamawe meupe. Kuuangalia vizuri ni yale mawe meupe wahuni walinipiga walaaniwe sana washenzi wale. Wateja wote wakanikimbia.
Nkajipanga tena nafika mashineni kuchukua mzigo nakutana na madalali wengi sana nkaona hii biashara pasua kichwa nkaachana nayo
Kwa mlio wahi kukumbana na umafia kwenye nafaka njooni hapa mtoe ushuhuda.