SoC01 “Asbestos” kemikali yenye madhara makubwa kiafya iliyosahaulika katika mazingira yetu

Stories of Change - 2021 Competition

genman

Member
Jul 14, 2021
37
102
ASBESTOS NI NINI?
Asbestos ni madini yanayochimbwa ardhini kama madini mengine. Kwa miaka iyoyopita asbsestos ilikuwa na bei nzuri katika soko la dunia kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi katika viwanda. Tanzania asbestos inapatikana Ikorongo (Musoma), mbembe (Morogoro), Rubeho(Mpwapwa) na Haneti (Dodoma) lakini madini haya hayakuchimbwa kutokuwa na soko na hii ilitokana na kuzuiliwa kwa matumizi yake katika nchi mbalimbali duniani.(1)

KWA NINI ASBESTOS NI HATARI?
Asbestos ni mojawapo ya chemikali au taka hatarishi kama ilivyoelezwa katika repoti ya Sensa ya Mazingira Tanzania bara ya 2017,

(2) na katika report ya Mpango wa Taifa wa uthibiti wa taka ngumu Tanzania ya mwaka 2018.
(3) Asbestos ni hatari kwa sababu huwa ina uwezo wa kuvunjika kwenye vinyuzi vidogo sana ambavyo hunasa kwenye njia ya hewa kwa muda mrefu. Vinyuzinyuzi hivi vidogo huendelea kuingia kwenye njia ya hewa kadiri mtu anavyozidi kupumua na baadae hufika kwenye njia ya mapafu. vinyuzivinyuzi vikitua kwenye mapafu huweza kusababisha madhara kama vile kansa ya mapafu, asbestosis (seli za mapafu kudhurika) na “mesothelioma” kansa ya mfuko wa mapafu
(4). Kansa ya mapafu huweza kutokea ndani ya mwaka mmoja kwa mtu aliyepo katika mazingira yenye asbestos lakini pia yaweza kuchukua miaka 10 na zaidi kwa mtu kupata madhara.
(5)Kiasi kidogo sana cha asbestos huweza usababisha ugonjwa wa mesothelioma. Wanafamilia wa wafanyakazi wanaofanya kazi sehemu zenye asbestos waliweza kupata ugonjwa huu kutokana na mabaki ya asbestos katika nguo zao(5).Sio kila mtu aliye katika mazingira yenye asbestos anaweza kupata magonjwa yatokanayo na asbestos. Ingawa mtu yeyote aliye katika mazingira yenye asbestos ana uwezeano mkubwa wa kupata magonywa yanayosababishwa na asbestos. Magonjwa yatokanayo na asbestos ni vigumu kuyatibu na ni vigumu kupona.

Hivyo ni muhimu zaidi kujizuia kuwa katika mazingira yenye asbestos.

KWA NAMNA GANI VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS HUINGIA HEWANI?
Vinyuzinyuzi vya asbestos huingia hewani wakati vifaa au vitu vilivyotengenezwa kwa asbestos vinapoharibika, kusuguana kwa kusogezwasogezwa au kuondolewa sehemu bila uangalifu. Asbestos inaposagika haitoi vumbi la kawaida, hutoa vinyuzinyuzi vidogo sana ambavyo siyo rahisi kuviona, kuhisi au kupata ladha/harufu yake. Kuna vifaa maalum ambavyo huweza utumika kugundua uwepo wa vinyuzinyuzi vya asbestos kwenye hewa.

Mtu yeyote ambaye yupo katika mazingira yenye vinyuzinyuzi hivi huweza kuvipumua na kuingia katika mfumo wake wa hewa. Madhara ambayo humtokea mtu hutegemea kiasi cha vinyuzinyuzi kilichopo hewani, muda ambao huyo mtu amekaa katika hayo mazingira na uwepo wa chemikali nyinginezo. Pia madhara hutofautiana kutokana na umri, jinsia, lishe, kinga ya mwili, mtindo ya maisha na afya ya mtu kwa ujumla.4)

UNAWEZA KUJUA KAMA UMEPUMUA VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS?
Wataalam wanasema ni vigumu sana kujua kama umeathirika na vinyuzinyuzi vya asbestos kwa sababu havisababishi kupiga chafya au kukohoa mara na havina madhara kwenye ngozi.

KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUJUA UMEATHIRIKA NA ASBESTOS?
Njia inayotumika kujua kama umeathirika na asbestos ni x-ray ya kifua au CAT scan. X-ray hutumika kugundua dalili za mwanzo za magonjwa yanayosababishwa na asbestos.

ASBESTOS INAPATIKANA WAPI KATIKA MAZINGIRA YETU?
Asbestos ipo kwa kiasi kikubwa Tanzania kwani vitu vyenye asbestos vinapatikana sehemu mbalimbali Tanzania nzima. Asbestos ilitumika katika kuezeka nyumba, kutengenezea mabomba, nguzo, vifaa vya umeme na vitu vingine vingi. Asbestos ilipendwa sana kutumika kwa sababu ni ngumu, haiozi au kupata kutu ikilowa pia haishiki moto. Hadi sasa asbestos iliyotumika miaka mingi iliyipita bado ipo katika mazingira yetu. Asbestos inapatikana katika majengo mengi ya zamani ya serikali kama vile ya shule na na hospitali na ya watu binafsi. Wananchi wameendelea kutumia mabaki ya bati za asbestos katika kuweka uzio na kujengea mabanda ya mifugo. Pia kuna mabomba yaliyotengenezwa kwa asbestos yamezikwa ardhini. Haya yalitumika katika mifumo ya maji safi na maji taka ambayo kwa sasa imekufa na haitumiki tena.

IMG_20210729_040758.jpg

Mabomba ya asbestos yaliyofukuliwa katika eneo la ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili Dar es Salaam.

Asbestos imetumika sana katika kuezeka nyumba Tanzania. Katika report ya Makazi na Hali ya Jamii Kiuchumi Tanzania Bara (Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland) ya mwaka 2014 inaonesha kwamba asbestos ipo kwa asilimia 0.3% katika uezekaji wa majengo Tanzania bara ukilinganisha na mabati, zege na vigae6. Watu huvuna maji ya matumizi ya nyumbani katika maezeko haya ya asbestos. Hii ni kutokana kukosekana kwa elimu ya madhara ya asbestos katika jamii.

Screenshot_20210714-133918.jpg

Nyumba ambayo imeezekwa kwa asbestos
Chanzo: British lung cancer foundation

Kwa sasa haijalishi upo sehemu gani, kwa sababu katika mazingira yetu kuna vitu vingi au mabaki ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa asbestos. Hivyo mabaki ya asbestos yapo kwa kiasi kikubwa katika udongo. Pia watanzania wengi hawana uelewa kuhusu madhara ya asbestos hivyo wamekuwa wakikaa nazo katika mazingira yao bila kujua madhara yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia vitu vyenye asbestos bila kujua hivyo kutochukua tahadhari yoyote.

IMG_20210728_160828.jpg

Bati za asbestos zilizoaribika zikiwa zimetupwa hovyo eneo la Mbagala

KWA NAMNA GANI ASBESTOS INAWEZA KUONDOLEWA KATIKA MAZINGIRA?
Katika nchi nyingi zilizoendelea kuna makampuni kadhaa yanayofanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira. Kampuni hizo huwa na wataalamu na vifaa vya kugundua asbestos katika mazingira. Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi huajiri kampuni hizi kuondoa asbestos katika mazingira yao.

JUHUDI ZA MATAIFA DUNIANI KUONDOA ASBESTOS KATIKA MAZINGIRA
Shirika la kazi duniani lilifanya mkutano wa makubaliano ya kimataifa mwaka 1986 ya kuthibiti uwepo wa asbestos katika mazingira. Nchi kadhaa kama vile Uganda na Zimbabwe ziliridhia makubaliano hayo lakini Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaridhia katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kwa nchi nyingi kwa miaka kadhaa wamekuwa na kampuni mbalimbali ambazo hufanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufanya hivyo.

HITIMISHO
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kumekuwa na maradhi mengi yatokanayo na taka hatarishi ambayo yanapunguza umri wa watu kuishi. Ni vyema serikali hasa kupitia vyombo vyake kama vile NEMC ikaongeza mikakati ya kuthibiti taka hatarishi hasa zilizosahaulika kama asbestos ili kulinda afya za watanzania. Wananchi wanatakiwa wapate elimu ya uelewa wa taka zote hatarishi ambazo zinapatikana katika mazingira yao na namna ya kujikinga nazo. Pia kuwe na mkakati wa kuondoa asbestos katika mazingira yetu. Juhudi hizi zikifanyika zitasaidia kulinda kizazi hiki na vijavyo.

REJEA
1. Jordan, P 1990. Mineral Industry Tanzania. Institute of Mineral Research of Zimbabwe. Report Number 119
2. United Republic of Tanzania, 2017, National Environment Statistics Report, Tanzania Mainland
3. United Republic of Tanzania, 2018, The National Solid Waste Management Strategy
4. Minnesota Department of Health. Environmental Health Division. Asbestos
https://www.health.state.mn.us/communities/environment/asbestos/homeowner/heffects.html
5. Boffetta P. 1998. Health effects of asbestos exposure in humans: a quantitative assessment. Med Lav.
6. United Republic of Tanzania, 2014, Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland.
 
Asante
Wazo lako ni zuri sana
Ila sasa changamoto ipo ivi
Tatizo linaanzia mbali kumbuka haya ni madini yanayochimbwa hivyo tatizo litaanzia mgodini kwa wale wachimbaji lazima wataathirika na vumbi litokanalo na uchimbaji na hata wakijikinga sana kumbuka vumbi linaweza kuchukuliwa na upepo na kwenda kuwaathiri watu wengine. Pili madini haya yakishachimbwa yatapelekwa kiwandani ambapo pia wakati wa kuchakata vumbi linaweza kuwaathiri wafanyakazi. Wafanyakazi wa viwandani ndio walikuwa waathirika wakubwa kwa vumbi la asbestos kuliko hata waliotumia bidhaa za asbestos. Nadhani kutokana na haya ndio maana wazungu wakakosa mbinu mbadala na kuamua kuachana na asbestos kabisa
asante sana mchangiaji
Asante sana Mkuu kwa kujibu swali langu haraka.

Kwa wale wachimbaji wa dhahabu nasikia hata almasi kuna kemikali ikimwagiwa udongo wenye madini hayo, madini ujikusanya pamoja badala ya kusambaa.

Mbali na mbinu nyingine kama kumwaga maji ama nyunyuzia maji kwenye migodi hiyo kufanya vumbi lipotee wahandisi na wana kemia wetu hawawezi kufanya jambo kama hili?

Pia najulishwa hata kwenye kuboresha maji safi ya kunywa kuna kemikali inakusanya vumbi lote na maji yanakuwa meupe! Hizi mbinu unazionaje!?
 
Hapo umesema jambo ishu ni teknologia hapo
 
Hizi bati nakumbuka zamani kuna Tangazo la biashara RTD wakisifia sana watu wezeke kwa Mabati ya Asbestors and me sijawahi yapenda sababu yakichakaa ukipanda kwenye paa unalo waeza tumbukia... Kwenye Stoo yetu imeezekwa na hayo Mabati na kuna sehemu Nazi iliangukia ikapasua bati moja pande kubwa...

Navyoyaelewa Tanzania yalitumika sana enzi zake yakisifiwa kutopata kutu.
 
Sijawahi kujua hili!
Utoto wangu wote hadi naondoka kwa wazazi mwaka 1999 nimeishi kwenye nyumba za kota zilizoezekwa kwa mabati ya asbestos. Ni eneo lenye mamia ya nyumba na by then zilikuwa chini ya serikali kabla ya privatization ya 1990s. Na naamini hadi sasa bado nyumba zile zimeezekwa na mabati yenye haya madini.😞
Ahsante
 
Umenikumbusha mbali mno kwenye somo la pharmacology, asante kwa elimu hii nzuri iliyokidhi viwango. Barikiwa sana mleta mada
 
ASBESTOS NI NINI?
Asbestos ni madini yanayochimbwa ardhini kama madini mengine. Kwa miaka iyoyopita asbsestos ilikuwa na bei nzuri katika soko la dunia kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi katika viwanda. Tanzania asbestos inapatikana Ikorongo (Musoma), mbembe (Morogoro), Rubeho(Mpwapwa) na Haneti (Dodoma) lakini madini haya hayakuchimbwa kutokuwa na soko na hii ilitokana na kuzuiliwa kwa matumizi yake katika nchi mbalimbali duniani.(1)

KWA NINI ASBESTOS NI HATARI?
Asbestos ni mojawapo ya chemikali au taka hatarishi kama ilivyoelezwa katika repoti ya Sensa ya Mazingira Tanzania bara ya 2017,(2) na katika report ya Mpango wa Taifa wa uthibiti wa taka ngumu Tanzania ya mwaka 2018.(3)
Asbestos ni hatari kwa sababu huwa ina uwezo wa kuvunjika kwenye vinyuzi vidogo sana ambavyo hunasa kwenye njia ya hewa kwa muda mrefu. Vinyuzinyuzi hivi vidogo huendelea kuingia kwenye njia ya hewa kadiri mtu anavyozidi kupumua na baadae hufika kwenye njia ya mapafu. vinyuzivinyuzi vikitua kwenye mapafu huweza kusababisha madhara kama vile kansa ya mapafu, asbestosis (seli za mapafu kudhurika) na “mesothelioma” kansa ya mfuko wa mapafu(4). Kansa ya mapafu huweza kutokea ndani ya mwaka mmoja kwa mtu aliyepo katika mazingira yenye asbestos lakini pia yaweza kuchukua miaka 10 na zaidi kwa mtu kupata madhara.(5)
Kiasi kidogo sana cha asbestos huweza usababisha ugonjwa wa mesothelioma. Wanafamilia wa wafanyakazi wanaofanya kazi sehemu zenye asbestos waliweza kupata ugonjwa huu kutokana na mabaki ya asbestos katika nguo zao(5).
Sio kila mtu aliye katika mazingira yenye asbestos anaweza kupata magonjwa yatokanayo na asbestos. Ingawa mtu yeyote aliye katika mazingira yenye asbestos ana uwezeano mkubwa wa kupata magonywa yanayosababishwa na asbestos. Magonjwa yatokanayo na asbestos ni vigumu kuyatibu na ni vigumu kupona. Hivyo ni muhimu zaidi kujizuia kuwa katika mazingira yenye asbestos.

KWA NAMNA GANI VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS HUINGIA HEWANI?
Vinyuzinyuzi vya asbestos huingia hewani wakati vifaa au vitu vilivyotengenezwa kwa asbestos vinapoharibika, kusuguana kwa kusogezwasogezwa au kuondolewa sehemu bila uangalifu. Asbestos inaposagika haitoi vumbi la kawaida, hutoa vinyuzinyuzi vidogo sana ambavyo siyo rahisi kuviona, kuhisi au kupata ladha/harufu yake. Kuna vifaa maalum ambavyo huweza utumika kugundua uwepo wa vinyuzinyuzi vya asbestos kwenye hewa. Mtu yeyote ambaye yupo katika mazingira yenye vinyuzinyuzi hivi huweza kuvipumua na kuingia katika mfumo wake wa hewa. Madhara ambayo humtokea mtu hutegemea kiasi cha vinyuzinyuzi kilichopo hewani, muda ambao huyo mtu amekaa katika hayo mazingira na uwepo wa chemikali nyinginezo. Pia madhara hutofautiana kutokana na umri, jinsia, lishe, kinga ya mwili, mtindo ya maisha na afya ya mtu kwa ujumla.4)

UNAWEZA KUJUA KAMA UMEPUMUA VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS?
Wataalam wanasema ni vigumu sana kujua kama umeathirika na vinyuzinyuzi vya asbestos kwa sababu havisababishi kupiga chafya au kukohoa mara na havina madhara kwenye ngozi.

KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUJUA UMEATHIRIKA NA ASBESTOS?
Njia inayotumika kujua kama umeathirika na asbestos ni x-ray ya kifua au CAT scan. X-ray hutumika kugundua dalili za mwanzo za magonjwa yanayosababishwa na asbestos.

ASBESTOS INAPATIKANA WAPI KATIKA MAZINGIRA YETU?
Asbestos ipo kwa kiasi kikubwa Tanzania kwani vitu vyenye asbestos vinapatikana sehemu mbalimbali Tanzania nzima. Asbestos ilitumika katika kuezeka nyumba, kutengenezea mabomba, nguzo, vifaa vya umeme na vitu vingine vingi. Asbestos ilipendwa sana kutumika kwa sababu ni ngumu, haiozi au kupata kutu ikilowa pia haishiki moto. Hadi sasa asbestos iliyotumika miaka mingi iliyipita bado ipo katika mazingira yetu. Asbestos inapatikana katika majengo mengi ya zamani ya serikali kama vile ya shule na na hospitali na ya watu binafsi. Wananchi wameendelea kutumia mabaki ya bati za asbestos katika kuweka uzio na kujengea mabanda ya mifugo. Pia kuna mabomba yaliyotengenezwa kwa asbestos yamezikwa ardhini. Haya yalitumika katika mifumo ya maji safi na maji taka ambayo kwa sasa imekufa na haitumiki tena.
View attachment 1872905
Mabomba ya asbestos yaliyofukuliwa katika eneo la ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili Dar es Salaam.

Asbestos imetumika sana katika kuezeka nyumba Tanzania. Katika report ya Makazi na Hali ya Jamii Kiuchumi Tanzania Bara (Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland) ya mwaka 2014 inaonesha kwamba asbestos ipo kwa asilimia 0.3% katika uezekaji wa majengo Tanzania bara ukilinganisha na mabati, zege na vigae6. Watu huvuna maji ya matumizi ya nyumbani katika maezeko haya ya asbestos. Hii ni kutokana kukosekana kwa elimu ya madhara ya asbestos katika jamii.
View attachment 1872909
Nyumba ambayo imeezekwa kwa asbestos
Chanzo: British lung cancer foundation

Kwa sasa haijalishi upo sehemu gani, kwa sababu katika mazingira yetu kuna vitu vingi au mabaki ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa asbestos. Hivyo mabaki ya asbestos yapo kwa kiasi kikubwa katika udongo. Pia watanzania wengi hawana uelewa kuhusu madhara ya asbestos hivyo wamekuwa wakikaa nazo katika mazingira yao bila kujua madhara yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia vitu vyenye asbestos bila kujua hivyo kutochukua tahadhari yoyote.
View attachment 1872912
Bati za asbestos zilizoaribika zikiwa zimetupwa hovyo eneo la Mbagala

KWA NAMNA GANI ASBESTOS INAWEZA KUONDOLEWA KATIKA MAZINGIRA?
Katika nchi nyingi zilizoendelea kuna makampuni kadhaa yanayofanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira. Kampuni hizo huwa na wataalamu na vifaa vya kugundua asbestos katika mazingira. Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi huajiri kampuni hizi kuondoa asbestos katika mazingira yao.

JUHUDI ZA MATAIFA DUNIANI KUONDOA ASBESTOS KATIKA MAZINGIRA
Shirika la kazi duniani lilifanya mkutano wa makubaliano ya kimataifa mwaka 1986 ya kuthibiti uwepo wa asbestos katika mazingira. Nchi kadhaa kama vile Uganda na Zimbabwe ziliridhia makubaliano hayo lakini Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaridhia katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kwa nchi nyingi kwa miaka kadhaa wamekuwa na kampuni mbalimbali ambazo hufanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufanya hivyo.

HITIMISHO
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kumekuwa na maradhi mengi yatokanayo na taka hatarishi ambayo yanapunguza umri wa watu kuishi. Ni vyema serikali hasa kupitia vyombo vyake kama vile NEMC ikaongeza mikakati ya kuthibiti taka hatarishi hasa zilizosahaulika kama asbestos ili kulinda afya za watanzania. Wananchi wanatakiwa wapate elimu ya uelewa wa taka zote hatarishi ambazo zinapatikana katika mazingira yao na namna ya kujikinga nazo. Pia kuwe na mkakati wa kuondoa asbestos katika mazingira yetu. Juhudi hizi zikifanyika zitasaidia kulinda kizazi hiki na vijavyo.

REJEA
1. Jordan, P 1990. Mineral Industry Tanzania. Institute of Mineral Research of Zimbabwe. Report Number 119
2. United Republic of Tanzania, 2017, National Environment Statistics Report, Tanzania Mainland
3. United Republic of Tanzania, 2018, The National Solid Waste Management Strategy
4. Minnesota Department of Health. Environmental Health Division. Asbestos
https://www.health.state.mn.us/communities/environment/asbestos/homeowner/heffects.html
5. Boffetta P. 1998. Health effects of asbestos exposure in humans: a quantitative assessment. Med Lav.
6. United Republic of Tanzania, 2014, Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland.

Hili bandiko ni zuri sana. Sijui ni kwanini hata sikuliona mapema.

Mafundi wa magari mnaofanya Brake service, Lile vumbi linalotokana na Brake linings za shoes au Pads limecontain asbestos.

Kwa mazingira yalivyo maeneo mengi huenda watu wanalivuta au kulishika. Hii inaweza kuwaletea madhara.
 
Kweli kabisa kaka tuna uhaba sana wa elimu ya afya na pia wengi hatujali afya zetu
 
Je kuna utafiti juu ya hili uliofanyika nchini kuonyesha madhara haya ya asbestos?
Mfano
1. Maeneo yenye nyumba hizi hususani, shule na vyuo vya zamani Tz watu wanaozunguka eneo hilo hu ripoti magonjwa gani kwa takwimu zilo hosp za eneo hilo? Au kanza ya mapafu iko kiwango gani na kwa watu wa maeneo yapi?

2. Je wakaaji wa maeneo ya migodi ya asbestos husumbuliwaliwa na ugonjwa unaoambanatana na madhara ya asbestos zaidi au la?

Nje ya utafiti yatakuwa maandiko ya wazungu walioniambia nisile Samuli ina cholestol wakati wazee wamezeeka wakila bila madhara yoyote
 
Wazungu waongo tu hamna lolote walifanya Industrial revolution ili kutuletea bidhaa feki zenye limitation ya mda kuisha.Mi kama kuna mtu mwenye mabati hayo ya asbestos awasiliane na mimi nayahitaji.Make hii dunia kila kitu ni sumu no where to escape,Asbestos chama la wana tuishi humo humo.
 
Ni miaka mingi saaa tangu asbestos itangazwe kuwa ni hatari. Watu wengi wametumia vifaa vya asbestos hasa mabati na mabomba ya maji safi na taka kama mwandishi anavyoeleza.

Familia nyingi hapa Tz zimeishi mazingira yenye matumizi ya asbestos.
Kwasababu ya umasikini wetu huenda tunaweza kuja na majibu mengine tofauti kuhusu madhara ya asbestos.

Ipo haja ya wataalam wetu kujiridhisha na madhara tajwa yatokanayo na asbestos.
 
asante kwa maoni yako
1. Kwa sasa hatuna machimbo ya asbestos Tanzania ila tulitumia bidhaa mbalimbali ambazo zilitengenezwa kwa absestos kwa miaka mingi iliyopita
2. Tanzania na dunia kwa ujumla inahitaji tafiti nyingi kwa matatizo mengi yanayotukabili na tafiti hizi zinahitaji hela hivyo tafiti nyingi bado hazijafanyika kwa sababu ya ufinyu wa hela. Ila wazungu wameweza kufanya tafiti nyingi sana kuendana na uwezo wao na wakati mwingine tunatumia tafiti zao kutatua matatizo yetu. sio kila kitu kutoka kwao ni cha kubeza kwani tunatumia hata madawa kutoka kwao
Soma jibu la waziri bungeni kipindi cha nyuma kuhusu tafiti za asbestos keenya link hii👇

Soma na hizi pia👇
habarileo.co.tz/habari/majengo-yenye-asbestos-yafanyiwa-tathmini.aspx

Ni miaka mingi saaa tangu asbestos itangazwe kuwa ni hatari. Watu wengi wametumia vifaa vya asbestos hasa mabati na mabomba ya maji safi na taka kama mwandishi anavyoeleza.

Familia nyingi hapa Tz zimeishi mazingira yenye matumizi ya asbestos.
Kwasababu ya umasikini wetu huenda tunaweza kuja na majibu mengine tofauti kuhusu madhara ya asbestos.

Ipo haja ya wataalam wetu kujiridhisha na madhara tajwa yatokanayo na asbestos.
kweli kabisa
 
Asbestos ni common cause ya bronchiogenic mesothelioma hii ni cancer

Na tuna hard asbestos na soft asbestos

Inayoleta madhara zaidi ni crocodite asbestos au tunaiita blue asbestos

Pia mtu mwenye asbestosis anaweza pata pleural calcification
 
Wazungu waongo tu hamna lolote walifanya Industrial revolution ili kutuletea bidhaa feki zenye limitation ya mda kuisha.Mi kama kuna mtu mwenye mabati hayo ya asbestos awasiliane na mimi nayahitaji.Make hii dunia kila kitu ni sumu no where to escape,Asbestos chama la wana tuishi humo humo.
Si ajabu
Zebaki/mercury ni hatari lakini watu wanaishika kwa mikono wanaitumia kusafishia dhahabu
 
Asbestos ni common cause ya bronchiogenic mesothelioma hii ni cancer

Na tuna hard asbestos na soft asbestos

Inayoleta madhara zaidi ni crocodite asbestos au tunaiita blue asbestos

Pia mtu mwenye asbestosis anaweza pata pleural calcification
Asante kwa elimu mkuu
 
Asante kwa elimu mkuu
Sio asbestos tu tuna vitu vingine kama vile beryllium vina madhara makubwa kwa jamii
Pia silicone inayosababisha silicotic nodule kwenye mapafu so unaweza kwenda kusoma zaidi ukaleta mada zngne kama hizo
 
ASBESTOS NI NINI?
Asbestos ni madini yanayochimbwa ardhini kama madini mengine. Kwa miaka iyoyopita asbsestos ilikuwa na bei nzuri katika soko la dunia kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi katika viwanda. Tanzania asbestos inapatikana Ikorongo (Musoma), mbembe (Morogoro), Rubeho(Mpwapwa) na Haneti (Dodoma) lakini madini haya hayakuchimbwa kutokuwa na soko na hii ilitokana na kuzuiliwa kwa matumizi yake katika nchi mbalimbali duniani.(1)

KWA NINI ASBESTOS NI HATARI?
Asbestos ni mojawapo ya chemikali au taka hatarishi kama ilivyoelezwa katika repoti ya Sensa ya Mazingira Tanzania bara ya 2017,(2) na katika report ya Mpango wa Taifa wa uthibiti wa taka ngumu Tanzania ya mwaka 2018.(3)
Asbestos ni hatari kwa sababu huwa ina uwezo wa kuvunjika kwenye vinyuzi vidogo sana ambavyo hunasa kwenye njia ya hewa kwa muda mrefu. Vinyuzinyuzi hivi vidogo huendelea kuingia kwenye njia ya hewa kadiri mtu anavyozidi kupumua na baadae hufika kwenye njia ya mapafu. vinyuzivinyuzi vikitua kwenye mapafu huweza kusababisha madhara kama vile kansa ya mapafu, asbestosis (seli za mapafu kudhurika) na “mesothelioma” kansa ya mfuko wa mapafu(4). Kansa ya mapafu huweza kutokea ndani ya mwaka mmoja kwa mtu aliyepo katika mazingira yenye asbestos lakini pia yaweza kuchukua miaka 10 na zaidi kwa mtu kupata madhara.(5)
Kiasi kidogo sana cha asbestos huweza usababisha ugonjwa wa mesothelioma. Wanafamilia wa wafanyakazi wanaofanya kazi sehemu zenye asbestos waliweza kupata ugonjwa huu kutokana na mabaki ya asbestos katika nguo zao(5).
Sio kila mtu aliye katika mazingira yenye asbestos anaweza kupata magonjwa yatokanayo na asbestos. Ingawa mtu yeyote aliye katika mazingira yenye asbestos ana uwezeano mkubwa wa kupata magonywa yanayosababishwa na asbestos. Magonjwa yatokanayo na asbestos ni vigumu kuyatibu na ni vigumu kupona. Hivyo ni muhimu zaidi kujizuia kuwa katika mazingira yenye asbestos.

KWA NAMNA GANI VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS HUINGIA HEWANI?
Vinyuzinyuzi vya asbestos huingia hewani wakati vifaa au vitu vilivyotengenezwa kwa asbestos vinapoharibika, kusuguana kwa kusogezwasogezwa au kuondolewa sehemu bila uangalifu. Asbestos inaposagika haitoi vumbi la kawaida, hutoa vinyuzinyuzi vidogo sana ambavyo siyo rahisi kuviona, kuhisi au kupata ladha/harufu yake. Kuna vifaa maalum ambavyo huweza utumika kugundua uwepo wa vinyuzinyuzi vya asbestos kwenye hewa. Mtu yeyote ambaye yupo katika mazingira yenye vinyuzinyuzi hivi huweza kuvipumua na kuingia katika mfumo wake wa hewa. Madhara ambayo humtokea mtu hutegemea kiasi cha vinyuzinyuzi kilichopo hewani, muda ambao huyo mtu amekaa katika hayo mazingira na uwepo wa chemikali nyinginezo. Pia madhara hutofautiana kutokana na umri, jinsia, lishe, kinga ya mwili, mtindo ya maisha na afya ya mtu kwa ujumla.4)

UNAWEZA KUJUA KAMA UMEPUMUA VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS?
Wataalam wanasema ni vigumu sana kujua kama umeathirika na vinyuzinyuzi vya asbestos kwa sababu havisababishi kupiga chafya au kukohoa mara na havina madhara kwenye ngozi.

KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUJUA UMEATHIRIKA NA ASBESTOS?
Njia inayotumika kujua kama umeathirika na asbestos ni x-ray ya kifua au CAT scan. X-ray hutumika kugundua dalili za mwanzo za magonjwa yanayosababishwa na asbestos.

ASBESTOS INAPATIKANA WAPI KATIKA MAZINGIRA YETU?
Asbestos ipo kwa kiasi kikubwa Tanzania kwani vitu vyenye asbestos vinapatikana sehemu mbalimbali Tanzania nzima. Asbestos ilitumika katika kuezeka nyumba, kutengenezea mabomba, nguzo, vifaa vya umeme na vitu vingine vingi. Asbestos ilipendwa sana kutumika kwa sababu ni ngumu, haiozi au kupata kutu ikilowa pia haishiki moto. Hadi sasa asbestos iliyotumika miaka mingi iliyipita bado ipo katika mazingira yetu. Asbestos inapatikana katika majengo mengi ya zamani ya serikali kama vile ya shule na na hospitali na ya watu binafsi. Wananchi wameendelea kutumia mabaki ya bati za asbestos katika kuweka uzio na kujengea mabanda ya mifugo. Pia kuna mabomba yaliyotengenezwa kwa asbestos yamezikwa ardhini. Haya yalitumika katika mifumo ya maji safi na maji taka ambayo kwa sasa imekufa na haitumiki tena.
View attachment 1872905
Mabomba ya asbestos yaliyofukuliwa katika eneo la ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili Dar es Salaam.

Asbestos imetumika sana katika kuezeka nyumba Tanzania. Katika report ya Makazi na Hali ya Jamii Kiuchumi Tanzania Bara (Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland) ya mwaka 2014 inaonesha kwamba asbestos ipo kwa asilimia 0.3% katika uezekaji wa majengo Tanzania bara ukilinganisha na mabati, zege na vigae6. Watu huvuna maji ya matumizi ya nyumbani katika maezeko haya ya asbestos. Hii ni kutokana kukosekana kwa elimu ya madhara ya asbestos katika jamii.
View attachment 1872909
Nyumba ambayo imeezekwa kwa asbestos
Chanzo: British lung cancer foundation

Kwa sasa haijalishi upo sehemu gani, kwa sababu katika mazingira yetu kuna vitu vingi au mabaki ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa asbestos. Hivyo mabaki ya asbestos yapo kwa kiasi kikubwa katika udongo. Pia watanzania wengi hawana uelewa kuhusu madhara ya asbestos hivyo wamekuwa wakikaa nazo katika mazingira yao bila kujua madhara yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia vitu vyenye asbestos bila kujua hivyo kutochukua tahadhari yoyote.
View attachment 1872912
Bati za asbestos zilizoaribika zikiwa zimetupwa hovyo eneo la Mbagala

KWA NAMNA GANI ASBESTOS INAWEZA KUONDOLEWA KATIKA MAZINGIRA?
Katika nchi nyingi zilizoendelea kuna makampuni kadhaa yanayofanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira. Kampuni hizo huwa na wataalamu na vifaa vya kugundua asbestos katika mazingira. Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi huajiri kampuni hizi kuondoa asbestos katika mazingira yao.

JUHUDI ZA MATAIFA DUNIANI KUONDOA ASBESTOS KATIKA MAZINGIRA
Shirika la kazi duniani lilifanya mkutano wa makubaliano ya kimataifa mwaka 1986 ya kuthibiti uwepo wa asbestos katika mazingira. Nchi kadhaa kama vile Uganda na Zimbabwe ziliridhia makubaliano hayo lakini Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaridhia katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kwa nchi nyingi kwa miaka kadhaa wamekuwa na kampuni mbalimbali ambazo hufanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufanya hivyo.

HITIMISHO
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kumekuwa na maradhi mengi yatokanayo na taka hatarishi ambayo yanapunguza umri wa watu kuishi. Ni vyema serikali hasa kupitia vyombo vyake kama vile NEMC ikaongeza mikakati ya kuthibiti taka hatarishi hasa zilizosahaulika kama asbestos ili kulinda afya za watanzania. Wananchi wanatakiwa wapate elimu ya uelewa wa taka zote hatarishi ambazo zinapatikana katika mazingira yao na namna ya kujikinga nazo. Pia kuwe na mkakati wa kuondoa asbestos katika mazingira yetu. Juhudi hizi zikifanyika zitasaidia kulinda kizazi hiki na vijavyo.

REJEA
1. Jordan, P 1990. Mineral Industry Tanzania. Institute of Mineral Research of Zimbabwe. Report Number 119
2. United Republic of Tanzania, 2017, National Environment Statistics Report, Tanzania Mainland
3. United Republic of Tanzania, 2018, The National Solid Waste Management Strategy
4. Minnesota Department of Health. Environmental Health Division. Asbestos
https://www.health.state.mn.us/communities/environment/asbestos/homeowner/heffects.html
5. Boffetta P. 1998. Health effects of asbestos exposure in humans: a quantitative assessment. Med Lav.
6. United Republic of Tanzania, 2014, Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland.
Aisee! Shukrani Mkuu kwa kutujuza jambo hilo ili tuchukue tahadhari.
 
Back
Top Bottom