Akili ya binadamu

Morgan Fisherman

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
1,804
2,079
Natumai mko poa pamoja na hizi tozo.

Mind-body dualism hii ni dhana kwamba akili(mind) na mwili(body) wa binadamu ni vitu viwili tofauti kila kimoja kinajitegemea kivyake.Dhana hii ilikua maarufu katika karne ya 17 kutokana na mwanamahesabu wa ufaransa aitwaye René Descartes,alikua na msemo wa kilatin “Cogito, ergo sum,” kwa kiingereza ni "I think, therefore I am” kwa lugha nyepesi ntasema "You are not your mind, you are the one listening to it" yanii wewe sio akili yako wewe ni yule unaesikiliza akili inakwambia nini.

Akili(mind) inahusisha ufahamu (consciousness) hii inafanya akili igawanyike kwenye makundi makuu matatu hii dhanaria ilikuwepo kitambo lakini ilielezewa vizuri na mwanasaikolojia kutoka Austria,bwana Sigmund Freud.

Makundi ya akili ya binadamu
1.unconscious mind
2.subconscious mind na
3.conscious mind

1.UNCONSCIOUS MIND.

Akili hii imeundwa na hisia,tabia,mawazo,mihemko kwa ujumla kumbukumbu za zamani au za sasa ambazo mara nyingi huwa ni za kuogofya au za kututia aibu,hivyo tunazipotezea na tunaziweka nje ya ufahamu wetu tusiweze kuzikumbuka.

Ingawa hatujui uwepo wa kumbukumbuku hizi ila zina ushawishi mkubwa juu ya tabia zetu za kila siku,zinaweza kusababisha shida kadhaa, pamoja na
hasira,woga,tabia ya kuchaguachagua vitu(mfano chakula),mwingiliano mgumu wa kijamii na shida kwenye mahusiano.Freud aliamini kuwa wakati mwingine kumbukumbu hizi zilizofichwa hujidhihirisha kupitia ndoto na kuteleza kwa ulimi(ulimi hauna mfupa).

2. SUBCONSCIOUS MIND.

Akili hii imeundwa na kumbukumbu zote zinazohitajika kukumbukika kwa urahisi, kama tarehe ya siku yako ya kuzaliwa,inashikilia kumbukumbu tunazotumia kila siku, kama tabia na hisia.Pia hushughulika na kila kitu ambacho mwili wako unahitaji kufanya kazi vizuri, kutoka mfumo wa chakula hadi mfumo wa upumuaji hata unapokua umelala na pia ndio chanzo cha ndoto tunazoziota hata kama tukiwa tumelala na hatujitambui.

Subconscious mind mara nyingi huwa inahusishwa na imani kwani ina nguvu sana katika maisha ya binadamu, miujiza yote kama uponyaji huwa inatokea kwenye akili hii mtu anapoamini,kwasababu wazo lolote tunalopanda katika akili hii aidha baya au zuri kwa kurudiarudia siku moja litakuwa ukweli(maneno uumba) hivyo tunahitaji kuwa makini sana na mambo tunayofikiria na kuyaongea.Tukiwaza vitu hasi(negative) itatupelekea kutokuwa na furaha,afya bora na kutofaulu katika maisha yetu pia tukiwaza vitu chanya (positive) tutapata furaha,afya bora na utafanikiwa kwenye maisha yetu.

Kwa kuchukua udhibiti wa akili hii, tunaweza kuwa na uhakika wa kudhibiti tena maisha yetu na kufanikisha chochote tunachotaka. Hii ni kwa sababu wakati subconscious mind, conscious mind na mwili(body) zinapofanya kazi pamoja ili kufikia lengo moja, tunaweza kuamini kwamba lengo hilo litafanikiwa kivyovyote. Meditation ni njia rahisi zaidi inayoweza kutuunganisha na akili hii.

3. CONSCIOUS MIND.

Akili hii inahusisha vitu tunavyotambua na ambavyo tunavifikiria hivi sasa kwa mfano, unavyousoma huu uzi, sauti ya muziki unaosikiliza na kufanya mazungumzo.

Akiili hii ndio mlango wa taarifa kwa njia ya picha au sauti kutoka kwenye mazingira ya nje yanayomzunguka binadamu na kuzihifadhi kwenye akili nyingine za binadamu,pia ni kupitia akili hii ndio tunaweza kufikia subconscious mind na kuficha na kufukia kumbukumbu nyingine kwenye unconscious mind.

Fisherman.
 
mkuu umeishia hapo hapo au unaemdelea?

Anyway ninachoweza kukuambia mpaka sasa ni kwamba bado hujaifikia vizuri kuisoma akili ya mwanadmu, umeishia kusoma maandiko ya larne ya 17 ya akina Rene Descarte, Freud Sigmund n.k

Ni sawa na safari ya kutoka Dodoma mpaka Dar wewe umeishia kongwa bado hujafika sehemu unayotakiwa kufika, bado hujaelewa maana ya akili

Nitafafanua vizuri

Hapo zamani wanasayansi walikuwa wanajiuliza je akili ni nini (what is Mind?), what is Memory, what is emotions? Je zinahifadhiwa vipi kwenye mwili wa binadamu? Na hupatikana sehemu gani?

Wanasayansi mbali mbali wakaanza kufanya uchunguzi na tafiti mbali mbali, akiwemo rene discarte na Freud Sigmund wakawa wanakuja na nadharia mbali mbali
 
ni kweli sijaingia deep sana lakini mchango wako pia ni muhimu sana unaweza kutuelezea from your point of view.
 
Baadaye kuna daktari mmoja mtaalamu wa Neuroscience alimfanyia mtu upasuaji wa ubongo ili kuondoa uvimbe, alifanya upasuaji akamaliza akamruhusu mgonjwa aende nyumbani, baada ya siku kadhaa mgonjwa akarudishwa hospitali akilalamika kuwa anapoteza kumbu kumbu hawezi kukumbuka matukio ya miaka ya nyuma na amewasahau mpaka watoto wake,

Ndipo hapo huyo daktari akanga'mua kuwa kumbu kumbu huhifadhiwa kwenye sehemu ya ubongo wa kati sehemu aliyoiondoa wakati wa upasuaji ndiyo hiyo inayohusika na kumbukumbu, baada ya ugunduzi huo wakaona kuwa akili na kumbu kumbu zote zipo kwenye ubongo ambapo ni sehemu ya mwili wa binadamu kwa hiyo wakawa wame m proof wrong bwana RENE DISCARTE na duality theory yake aliyokuwa akidai akili inapatikana nje ya mwili wa binadamu
 
Baadae ndipo wanasayansi wote wakahamishia nguvu kuusoma ubongo kwa kutumia panya kama kiumbe wa majaribio, ndipo wakagundua kuwa kila sehemu ya ubongo inahusika na kazi flani, mfano ubongo wa nyuma kisogoni unahusika na kuona, ubongo wa kati usawa wa masikio unahusika na kusikia n.k

Tizama picha hapo chini
20210826_141604.jpg
 
Baadae wakaanza kutafuta kuelewa mechanism ya jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa kwenye ubongo,

wataalam wa molecular biology
Neuroscience
psychology
Radiology
chemistry
computer science

wote hawa walihusika hadi kuja kuelewa jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa, pia ndoto zinavyotokea ukilala
 
Eleza hapo namna ndoto inavyotokea maana kuna ndoto nyingine tunaota ni vituko.
 
Kwanza kabisa kabla sijaanza kuelezea majibu ya maswali inatakiwa tuangalie muumdo wa ubongo pamoja na mfumo wa fahamu

file-20181217-185240-at9go0.png

Hiyo picha hapo juu inaonyesha ubongo na uti wa mgongo, pia kuna matawi yanayochomoza kwa pembeni, kiufupi ni kwamba mwili woteunamfumo wa umeme, kila kiungo kina mfumo wa umeme, huu umeme unaspidi kubwa sana
Mfano
Ukigusa moto au kitu cha moto taarifa hupelekwa kwenye ubongo au uti wa mgongo kwa muda mfupi (robo ya robo ya sekunde) yaani kabla hata sekunde haijaisha taarifa ilishafika na kurudisha mrejesho kwenye misuli ya mkono
Hivyo basi ukigusa kitu cha moto unakiachia fasta. Kitendo hiki hutokea automatic
Angalia picha hapa chini
mechanism-action-nervous-system.jpg

Tuendelee,
Ubongo ni mkusanyiko wa neurons (vitu kama nyaya nyaya au kamba kamba vilivyojipanga katika mpangilio maalum kwa lugha ya kisasa mnaita connection)
Hizi neuron kazi yake ni kupitisha umeme.
Tizama picha
20210826_164043.jpg

Mkusanyiko wa hizi kamba kamba (neurons) ndio unaunda ubongo (hiyo sehemu nyekundu kwenye picha hapo chini ni ubongo (mkusanyiko wa kamba kamba) hiyo sehemu yenye njano ni uti wa mgongo na hizo kamba kamba za njano na blue ni matawi. Kiujumla mkusanyiko wote huo unaunda mfumo wa umeme ambao kimsingi ndio mfumo wa fahamu
20210826_163807.jpg

Ukisikia mtu kapalalaizi (palalysis) bassi jua mfumo wake wa umeme haufanyi kazi
 
Tuendelee,
Kamba kamba (neurons) zilizo ktk mpangilio maalum kwenye ubongo zinaunda kitu kinacho itwa circuit (kitu kama bala bala), yaani namaanisha hizo kamba kamba ukizipanga zikaunda uzi mrefu ndio circuit yenyewe.

kikawaida ubongo una mabilioni ya circuit (kamba kamba zilizojipanga kuunda kitu kama uzi), hizi circuit ukisema uzipange zote ziunde uzi mmoja basi zinaweza kufikia au kuzidi umbali wa kutoko duniani mpaka juani au mwezini.

jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa
Ukipita kwenye tope kisha ulaingia sebuleni kwenu ukanyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwako, utaacha nyayo au alama sakafuni, hicho unachokiacha sakafuni kinaitwa kumbu kumbu, hivyo basi ukipita mara nyingi zaidi na tope lako mguuni alama za unyayo zitakuwa nyingi zaidi, zitatengeneza kumbu kumbu nzito au ya kudumu mpaka siku utakayo amua kusafisha au kupiga deki

Hivyo hivyo kwenye ubongo, kila tukio hupita kwenye circuit ktk mfumo wa umeme, mfano ukiambiwa huyu ni shangazi circuit moja itapitisha umeme na kurekodi tukio lote, ukiambiwa huyu ni Ronaldo circuit ya pili itapitisha umeme na kurekodi, hivyo basi taarifa hurekodiwa kwa mfumo huo, siku ukiulizwa Ronaldo anafananaje, utaanza kumuelezea jinsi alivyo au kumchora kabisa sababu ulisharekodi picha yake au video kwenye circuit ya ubongo wako,

Binadamu tuna mabilioni ya circuit huwezi kuyajaza yote kwa kurekodi taarifa au matukio.​
 
Kama umesoma una degree au masters ya taaluma flani maana yake kwenye ubongo wako kuna circuit nyingi zilizo active zenye kumbu kumbu ya ma presentation, ma lecture, na vitabu mbali mbali vya taaluma husika, wakati huo huo wewe ni shabiki wa Arsenal, Mzazi, mwanachama wa CCM/CHADEMA yaani una ma circuit mengi . Mkusanyiko wa circuits ndio unaunda identity zako mbali mbali. Hizi circuits zitakuwa active siku zote mpaka siku utakayokufa,

Kwa siku matukio ni mengi ubongo unachoka sana kurekodi, pia hauwezi kurekodi kila kitu hivyo basi kuna vitu vitakuwa deleted ili kuupunguzia ubongo kazi. Oxygen na energy inayotumika ni nyingi sana. Kulala ni njia mojawapo ya kuupumzisha ubongo.
 
Tuendelee,
Kamba kamba (neurons) zilizo ktk mpangilio maalum kwenye ubongo zinaunda kitu kinacho itwa circuit (kitu kama bala bala), yaani namaanisha hizo kamba kamba ukizipanga zikaunda uzi mrefu ndio circuit yenyewe.

kikawaida ubongo una mabilioni ya circuit (kamba kamba zilizojipanga kuunda kitu kama uzi), hizi circuit ukisema uzipange zote ziunde uzi mmoja basi zinaweza kufikia au kuzidi umbali wa kutoko duniani mpaka juani au mwezini.

jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa
Ukipita kwenye tope kisha ulaingia sebuleni kwenu ukanyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwako, utaacha nyayo au alama sakafuni, hicho unachokiacha sakafuni kinaitwa kumbu kumbu, hivyo basi ukipita mara nyingi zaidi na tope lako mguuni alama za unyayo zitakuwa nyingi zaidi, zitatengeneza kumbu kumbu nzito au ya kudumu mpaka siku utakayo amua kusafisha au kupiga deki

Hivyo hivyo kwenye ubongo, kila tukio hupita kwenye circuit ktk mfumo wa umeme, mfano ukiambiwa huyu ni shangazi circuit moja itapitisha umeme na kurekodi tukio lote, ukiambiwa huyu ni Ronaldo circuit ya pili itapitisha umeme na kurekodi, hivyo basi taarifa hurekodiwa kwa mfumo huo, siku ukiulizwa Ronaldo anafananaje, utaanza kumuelezea jinsi alivyo au kumchora kabisa sababu ulisharekodi picha yake au video kwenye circuit ya ubongo wako,

Binadamu tuna mabilioni ya circuit huwezi kuyajaza yote kwa kurekodi taarifa au matukio.​
Endelee kushusha nondo mkuu...
 
Jinsi ndoto zinavyotokea
Kulala ni njia ya kupumzisha ubongo wako, hiki kitendo hutokea automatic, kumbuka circuits zako ziko active 24 hours, ili ubongo upumzike kinachofanyika ni circuits zinakuwa zinajizima kwa mtindo kama wa bulb inayofifia mwanga, na mara nyingi huwa zinajizima na kujiwasha kwa zamu.
Picha ya bulb

Hivyo basi unapokuwa umelala, wakati circuit zinajizima na kujiwasha bahati mbaya ikajiwasha ile yenye kumbu kumbu ya tendo la ndoa, wakati huo huo ikajiwasha pamoja na circuit ya kumbu kumbu ya shangazi, utajiona unafanya mapenzi na shangazi yako na unaweza kupiga bao kabisa ukajimwagia mbegu hapa jf mnaita kumwaga wazungu, 😃, na ukiamka utaanza kusema ni mapepo kumbe ubongo unajizima na kujiwasha ili kusubili oxygen na glucose nyingi iingie kwenye mzunguko wa damu (nishati).​

dim-and-bright-bulb-side-by-side-showing-comparison-of-dim-and-bright-GF9557.jpg
 
Tiger woods huwa anacheza gofu kwa imaginations, yaani anakaa peke yake sehemu anaanza ku imagine anacheza golf, Michael Jordan naye hucheza basketball kwa imagination, mfano wewe ndugu msomaji uanze kucheza draft kichwa kichwa bila draft wala kete kuwepo, yaani unalichezea kichwani unakula kete unaingia kingi mwendo wa one touch.

Huko ndio ku create future, wanaofanya Meditation hufanya kwa mtindo huu sema target ya lengo ni tofauti na anayecheza basket bsll au draft,

Meditation mfano wake halisi uanze kuimagine ule ugonjwa wako unaokusumbua unaanza kupona unajiona unapata nguvu, kuna watu wamepona kansa kwa mtindo huu.

NB: Mimi sio mtaalam wa meditation but siamini mambo ya kiroho ila issue za kucheza golf, draft au kuimagine nimeajiliwa niko napiga kazi naziunga mkono zinapunguza stress zinaongeza hamasa ya utafutaji zinatanua akili.

Kila mtu aishi apendavyo​
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom