Aisee kumbe Unywaji wa Pombe unaleta Raha namna hii?

Bush Dokta

JF-Expert Member
Apr 11, 2023
12,705
21,296
Ndio maana wanywaji wengi wanafanikiwa na hawapungukiwi.

Yaani utakuta Mtu yuko chakali kila siku na sio kwamba ana michongo mikali sana wala nini.

Ni kupitia kanuni ile ile kwamb Wanywaji hawapungikiwi. Hata kama hana kitu bado ana matumaini ya kupata.

Ukinywa Pombe hakuna usumbufu unajisikia raha tu muda wote hata kama una shida.

Hunaga shida na mtu hata Mama watoto au Mpenzi wako akichepuka we huna habari. Ni mambo mbwelele na hujali.

Pombe inafuta makosa mengi. Inakufanya una concentrate na Mision zako tu. Maana huna shida na mtu.

Kama we ni tajiri au maskini Mnywa pombe hayamhusu. Siku zote ana imani atapata.

Tunyweni bia aisee. Hata zile ngonjera za kataa ndoa zitaisha
 
Leo nimashangaa ramazani baada ya kunywa pombe
FB_IMG_1710350719371.jpg
 
Ndio maana wanywaji wengi wanafanikiwa na hawapungukiwi.

Yaani utakuta Mtu yuko chakali kila siku na sio kwamba ana michongo mikali sana wala nini...
hata kipindi cha sodoma na gomora ilikuwa hivihivi, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, kwa kifupi walikuwa wanakula bata, hadi siku ile waliposhitukia maji yameshajaa.

TITO 2:9 inasema,

11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.

Tunaamriwa kukataa uovu, ukiamka asubuhi kataa uovu, ukiwa kazini kataa uovu, ukiwa barabarani kataa uovu, popote ulipo kataa uovu, neema ipo nayo inatufundisha tukatae uovu kabisa, ili tuokolewe.
 
Ndio maana wanywaji wengi wanafanikiwa na hawapungukiwi.

Yaani utakuta Mtu yuko chakali kila siku na sio kwamba ana michongo mikali sana wala nini...
Pombe hainywewe shida ndugu,ukifanya hi vyo umekubali kushindwa kabla haujaanza harakati zako za mafanikio hata yale madogo zaidi ambayo unngeweza kuyafikia iwe ni kwenye pombe, vilevi vuta ama aina nyinginezo.

Ushauri kwenye kunywa ni kunywa kwa kuwajibika(drink responsibly) Kwenye kuvuta kwa vivuto rasmi ni kuwa kuvuta kunaweza kuwa sii salama kwa afya yako( cigarette smoking is dangerous to your health).Hivyo kikubwa ni akili kumkichwa🤔.Zakuambiwa changanyamoo na zakwaaaakooo🤸
 
Pombe hainywewe shida ndugu,ukifanya hi vyo umekubali kushindwa kabla haujaanza harakati zako za mafanikio hata yale madogo zaidi ambayo unngeweza kuyafikia iwe ni kwenye pombe,vilevi vuta ama aina nyinginezo, ushaauri kwenye kunywa ni kunywa kwa kuwajibika(drink responsibly) Kwenye kuvuta kwa vivuto rasmi ni kuwa kuvuta kunaweza kuwa sii salama kwa afya yako( cigarette smoking is dangerous to your health).Hivyo kikubwa ni akili kumkichwa🤔.Zakuambiwa changanyamoo na zakwaaaakooo🤸
Ngoja tuone
 
Mie nikiwaga bataka kulitafakari jambo kwa kina, huenda bar nakunywa serengeti lite taratibu peke yangu, nakaa meza ya peke yangu pembeniiii, isiwe bar ya makelele, aisee hapo napataga majibu yote. Nikishamaliza naweka ktk note ya simu yangu kwa mpangilio, nakazia na mdudu na ndizi za mwaisa za kuponda hapo napata kafriji ka kufutia simu janja yangu.
 
Back
Top Bottom