Acha kuremba, piga saundi wewe

Mbahili

Senior Member
Nov 28, 2016
185
283
Hakuna wanaume ambao wanakera wanawake kama wale wanaume ambao wanaremba kutongoza. Unakuta lijitu linamuonyesha dalili dada wa watu kuwa linampenda, linamtoa out, kumsifia kila siku, kumuangalia kimahaba na kila kitu. Binti anajitongoza mwenyewe, anamtambulisha mwanaume kwa wazazi wake huko kichwani, anajiozesha na wattoto anajizalisha ila lijamaa kimya.

Halafu jingine basi hata mwanamke akitaka kuwa na mtu mwingine, linakasirika, linanuna na kupunguza mawasiliano ila linategwa mpaka mwisho lakini halisemi nakupenda, halisemi chochote. Mwana mzima unajizungusha zungusha tu na mwanamke kama mpenzi wako lakini hufanyi maamuzi ya kumtongoza.

Hii mbali na kwamba inampotezea muda mwanamke lakini unawazibia riziki mabaharia wa kweli, acha hayo, mtongoze dada wa watu akubali acha kumchanganya na kama humtaki unataka mtu wa kuongozana naye na kujichekeshachekesha basi hembu muache nenda kajichekeshe na dada zako mbona na wao wako single!
 
Back
Top Bottom