Mdogo mdogo vipi wakati Russia aliianzisha mwenyewe vita na sasa amechoka?
Nani anataka kupigana vita muda mrefu?
Russia ameanzisha vita lakini hajui namna ya kuimaliza.
Bado hujajibu hoja.
Sote tunajua, huwezi kuwa mwanasheria kama hujasoma na kufuzu, hivyo neno mwanasheria limebeba usomi ndani yake.
Sasa nini mantiki ya kuitwa mwanasheria msomi?
Je, kuna wanasheria wasio wasomi?
Ndugu yangu Dar inabebwa na vitu viwili tu.
1. Bandari
2. Wingi wa watu.
Kumbuka tu, 35% ya pato la taifa linatokana na Bandari, na 10% ya watanzania wako Dar na kati yao 90% wanaishi mjini. Penye watu, penye mji, pana shughuli na pana pesa. Huwezi kulazimisha Arusha iwe na shughuli nyingi...
Karia muda wake unakwisha May, 2025. Na hatapaswa kugombea tena kwa mujibu wa katiba ya TFF. Mpaka kufikia mwakani muda wake utakapokuwa umekwisha Karia atakuwa amehudumu kwa miaka nane, ikiwq ni vipindi viwili vya miaka minne minne.
Kwa wale ambao hatukuwahi kumkubali Karia na kuchoshwa na...
Kipindi pekee ambacho Arusha ilipitia hali mbaya zaidi kiuchumi ni kipindi cha Covid, na hapo kabla kile kipindi cha Magufuli.
Lakini tangu huyu mama Samia aingie, flow ya pesa imeongezeka zaidi kupitia Utalii.
Mimi ni mdau wa Utalii, Arusha naijua lakini hicho unachokisema kuhusu Utalii ni uongo mkubwa. Mnyororo wa Utalii ni mrefu na mpana mnoo kwa jiji la Arusha, sidhani kama kuna mji hapa Tanzania wenye mnyororo unaokaribiana na huo. Kwa kifupi sana ukiondoa kodi za serikali (ambazo hazizidi 1/3 ya...
Mji ambao anaweza akauziwa kitu mchina, mzungu, mhindi, mjapani, mkenya, mnyarwanda, msomali au mjamaika bila shida yoyote, sasa wewe mndengereko kwanini usiuziwe kama una pesa?
Arusha ni mji wa pesa, ukiwa na pesa utauziwa au kununua chochote, ukiwa huna hela utakuwa na maneno mengi tu ukitaka...
Huku zenji huwa tunaangalia kama una sigida usoni, umevaa barakashea kichwani, kanzu, msuli au kobazi ili tukuuzie kitu au tununue kitu.
Kama unataka kujua au kujifunza ubaguzi hapa Tanzania basi njoo Zenji.
Mkataba wa umiliki wa Ziwa Nyasa ni mtata sana, na tukisema mkataba wa Kikoloni utumike vile vile ulivyo basi lile ziwa litafutika!
Ni kweli, kimkataba (toka mkoloni) Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa 100%. Lakini linapakana na nchi kadhaa ambapo kimataifa mpaka unapaswa kupita katika ya ziwa...
Hata Berlin Comference ulikuwa ni mkutano wa wahuni kujigawiwa bure bure, kienyeji, kiwizi na kitapeli maeneo ya Afrika, lakini kupitia comference hiyo hiyo ndio ikaifanya Tanganyika (Tanzania!) kumiliki mlima Kilimanjaro.
Yeye na genge lao la Sukuma gang walipiga copy serikali iliyopita na kula keki mpaka kujisaidia ovyo bahati mbaya copy yao ika expire, wahuni wa Msoga wakafuata, wakajaribu na kufanikiwa kupiga copy yao mpya na wanakula keki mpaka kuvimbiwa.
Pole Pole anaumia tu, atulie tu kwa sasa wahuni...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.